Kutoka Songea: Vodacom Premier League VPL, Majimaji Vs Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018 kufungwa leo, je nani kushika nafasi ya pili Azam FC au Yanga SC?

Vita ya kushuka daraja je nani kuungana na Njombe Majimaji ama Ndanda FC?.

View attachment 788342

Umeanza mpira kwa mashambulizi kwa pande mbili

06' Gooooooaal.. Marcel Kaheza anaandika bao la kwanza kwa kisigino upande wa Majimaji

Majimaji 1-0 Simba SC

15' Niyonzima anapiga shuti na kugonga mwamba..na beki kuutoa mpira na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Mashabiki ni wachache sana kwenye uwanja huu wa Majimaji, mjini Songea

25' VPL, Majimaji 1-0 Simba SC

Kaheza anakwenda, lakini Bukaba anafika na kuokoa mpira ule

Hatari lango la Majimaji .. Ni kona, inapigwa kona lakini MO anapiga nje na kuwa Goal Kick

35' Mchezaji Costa wa Simba anaonyesha kadi ya njano kwa mchezo mbaya

MO anakwenda na mpira aaaa Kona, inapigwa kona fupi. Lakini haikuzaa matunda

39' mpira wa adhabu kuelekea Simba SC, inapigwa lakini mabeki wanaokoa

40' Kaheza anakwenda. Kona inapigwa lakini golikipa Nduda anadaka

43' Rashid Juma anakwenda na mpira..lakini anaangushwa eneo la hatari. Na refa anaamuru ipigwe peinati kuelekea lango la Majimaji

44' Goooooooal..Goooooooal .. Haruna Niyonzima anaisawazishia Simba bao kwa mkwaju wa peinati

Majimaji 1-1 Simba SC

45' Naam mpira ni mapumziko uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma

Ambapo timu zote zimetoshana nguvu kwa 1-1 kwa kipindi hiki cha kwanza


Mpira umeanza kipindi cha pili. Hakuna mabadiliko kwa wachezaji kwa pande zote.

46' Majimaji wanapata kona. Lakini wanapoteza mpira ule na kuwa goal kick

50' Majimaji 1-1 Simba SC uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma

Anakwenda pale lakini golikipa wa Majimaji anatokea nakudaka

60' Kaheza anakwenda .. Hatari eneo la Simba SC .. Mpira unakwenda nje na kuwa goal kick

62' Simba wanakwenda sasa. Lakini Rashid anakuwa Offside.

Mapunda anakwenda pembeni ya uwanja. Lakini mabeki wanamtegea na kuwa Offside

67' Luzuio anakwenda na mpira..Jafar anaunawa na kuwa peinati

70' Gooooal laaaaaaaaaa golikipa Hashim Mussa anapangua mkwaju wa peinati wa Haruna Niyonzima

76' Kaheza anapiga free kick. Lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

81' Moses Kitandu anaingia. Mo Ibrahim anakwenda kwenye benchi

86' golikipa Nduda yuko chini anapatiwa matibabu baada ya kupata rabsha. Ameinuka mpira unaendelea

Mapunda anakwenda. Konaa, inapigwa kona golikipa anapangua na kuwa kona nyingine.

88' Inapigwa kona kuelekea Simba. Na mpira unatoka nje na kuwa Goal Kick

Simba SC wanakwenda kwa kasi kwenye lango la Majimaji .. Inapigwa mpira lakini unaokolewa.

90+4' Wakati wowote mpira utakuwa umemalizika

Naaam dakika 90' za mtanange wa VPL umemalizika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma ambapo timu zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya 1-1.

Kwa matokeo hayo Majimaji wameshuka daraja baada ya kushindwa kupata ushindi na Ndanda FC kuchomoza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Stand United hivyo Majimaji kuungana na Njombe

Asanteni kwa yote....Ghazwat
 
Mpira umeanza kwa mashambulizi ya makali
 
06' Gooooal, Kaheza anaipatia Majimaji bao la kwanza
 
22' VPL, Majimaji 1-0 Simba SC uwanja wa Majimaji mjini Songea
 
Ingekua hatujafungwa Mechi na Kagera Ingeuma leo kufungwa.Ila kwa kua tulipogwa kidude hata leo tukifungwa ni sawa tu.Ili hata tuwaokoe hawa WAVIMBA MACHO wasirudi walipopazoea
 
Updates: Kutoka Mtwara Ndanda FC 2-0 Stand United
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…