Tunajitapa tunakuza Kiswahili kiwe lugha ya kimataifa, hapa ukumbuni tuna washiriki 100, kati ya hao, washiriki 99 ni Waswahili Watanzania, mzungu ni mmoja, lakini tunazungumza Kiingereza!, hii live stream ya Kiingereza kuwatangazia Waswahili, kiukweli haijakaa poa!, ila lugha ya tourism na hospitality ni kizungu zaidi!, hata wadada zetu, ukimwambia "nakupenda" unakataliwa, ukimwambia "I love you" unakubaliwa!. Hata mama, ukimuita "mtoto" anakasirika kuwa umemtukana, ila mijibaba, mijitu mizima na wajukuu, inapoitwa "baby!", inafurahi!.
Kiukweli wakoloni wametufanya vibaya na lugha yao!.
P