Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Ukiwa nguzo muhimu katika ujenzi wa Taifa,napenda kwa heshima na taadhima kukualika kwenye mkutano maalum wa kutangaza nia yangu ya kuomba utumishi kuiongoza nchi katika nafasi ya Uraisi kupitia CCM.Karibu tuanze pamoja Tanzania Mpya,leo katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia saa 9 alasiri hadi 12 jioni. J MAKAMBA.

My take, ukiwa waziri au naibu waziri wa mawasiliano raha sana
 
Narudia tena na tena
Siwezi kukaa kwenye kituo cha bvr kwa saa 24 na siku ya kura kwa saa 12 kwa ajili ya kuipigia kura ccm ni heri siku hiyo isiwepo!!!
 
Comrade, watu hawamtaki Muhongo lakini wanaimba kumtaka kiongozi makini.Hakuna kiongozi makini zaidi ya Muhongo.Na kwa hilo nashawishika kuamini kuwa tatizo letu si Marais wala vyama vyao, bali sisi wenyewe tumekosa akili za utambuzi.

Haswaaa muhongo yuko makini na nikichwa sana sema basi tu nabii hakubaliki kwao!
 
Reactions: R.B
Huyu Jamaa ni Pure mnafiki na Muongo huwezi ukasema utafanya mambo yote kwa nchi hii.
 
Kulingana na hiyo hotuba aliyoibutubia inaonekana kwamba huyo akiwa rais gharama za maisha zitapanda hivyo hatufai.
Yeye awaachie tu akina Makongoro na Mhongo wao wachuane kwenye chama hicho cha CCM kwani wao hata mmoja akipita anaweza kuiongoza nchi.
 

Mzee mwenzangu I conquer with u...huyu dogo don play,na ameset very high bar kiasi kwamba hawa wakongwe wanaonekana kindergarten kids

Na wakizubaa tu dogo anawaacha mbali sana...dogo did the unthinkable aisee...kajipanga kwa kifupi na team yake
 
Naomba kuuliza, baada ya kukosa kuiwakilisha CCM hayo magari yanaenda kupakwa rangi upya au ni sticker ni za kubandua tu? Mmmmh!
 
Hawa watia nia waccm wanashangaza sana.. Wanaongelea mipango isiyo vipaumbele vya chama chao, ni vizuri wakaanza kuongelea vipaumbele vya chama kama ufisadi etc, waanze kutuambia wataiba kiasi gani kama tutawapa tena nchi
 
Naomba kuuliza, baada ya kukosa kuiwakilisha CCM hayo magari yanaenda kupakwa rangi upya au ni sticker ni za kubandua tu? Mmmmh!

Wanaenda kubadilisha rangi kwa mchina kwa kutumia kodi yako! shtuka
 
Ana historia ya kufanya cheating kwenye mtihani ilyopelekewa kufutiwa matokeo
 
ninachojua vita ni makongoro na rowasa tu tatizo siijui kesho ndio maana namuomba mungu anipe uhai nijue nani zaidi
 
Ewe mleta mada hii gas unayoiona inaletwa siyo ilyovumbulia leo na haina uwingi wa kuweza kusafirishwa nje na kuiletea nchi fedha za kigeni.

Kuvuna Gas kiutajiri ni kweli kabisa si chini ya miaka 10 kuanzia sasa.

Umeongea nini sasa?
 
huyu jamaa ni pure mnafiki na muongo huwezi ukasema utafanya mambo yote kwa nchi hii.

kasema ataunda baraza la viongozi wa madhehebu mbalimbali..je,tusio na dini tuhame nchi au hatutambui.huyu january hamna kitu
 
Wewe unaongelea songo songo gas.
Lakini gas ilivumbuliwa sasa huko mtwara bado hata kuanza kuichimba bado.
Kuna kazi ya kutafuta wawekezeji kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…