Kutoka Uturuki: Friendly Match, Simba SC yaichapa F.C.E Ksaifa mabao 3-1

Kutoka Uturuki: Friendly Match, Simba SC yaichapa F.C.E Ksaifa mabao 3-1

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mabingwa wa nchi ya Tanzania Simba Sports Club leo Agosti 4, 2018 imechapa bila huruma F.C.E. Ksaifa mabao 3-1 katika mchezo safi wa kirafiki uliofanyika kwenye dimba la Kartepe Green Park.

Simba ikionyesha kandanda safi na la kuvutia kwenye mchezo huo, ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa Emmanuel Okwi katika dakika ya 16' kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Emmanuel Okwi aliipatia tena bao Simba dakika ya 50' ambapo lilidumu kwa dakika 4 tu baada ya F.C.E. Ksaifa kuandika bao lao la kwanza katika dakika 54 kupitia kwa mchezaji Nader Al-krinsui.

Mshambuliaji matata Meddie Kagere alihitimisha ukurasa wa mabao katika dakika ya 87' akifunga bao la tatu, hivyo mchezo huo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 3 dhidi ya bao 1 la F.C.E. Ksaifa.
IMG_20180804_185656_458.jpg
 
Mabingwa wa nchi ya Tanzania Simba Sports Club leo Agosti 4, 2018 imechapa bila huruma F.C.E. Ksaifa mabao 3-1 katika mchezo safi wa kirafiki uliofanyika kwenye dimba la Kartepe Green Park.

Simba ikionyesha kandanda safi na la kuvutia kwenye mchezo huo, ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa Emmanuel Okwi katika dakika ya 16'. Hadi mapumziko Simba ilikuwa mbele ya bao hilo moja.

Emmanuel Okwi aliipatia tena bao Simba dakika ya 50' ambapo lilidumu kwa dakika 4 tu baada ya F.C.E. Ksaifa kuandika bao lao la kwanza katika dakika 54 kupitia kwa mchezaji Nader Al-krinsui.

Mshambuliaji matata Meddie Kagere alihitimisha ukurasa wa mabao katika dakika ya 87' akifunga bao la tatu hivyo mchezo huo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 3 dhidi ya bao 1 la F.C.E. Ksaifa.View attachment 827078
Mkuu, Umemsahau kusema F.C.E Ksaifa ni timu ya Palestine. Siyo club bingwa ya Morroco
 
Hata wanawake huwa wanasema hivyo kaba kamoja tu hako, baada ya wiki mbili anasema haoni siku zake.
Angalia kipimo kabla ya Kupiga kelele. Usilete mifano unrelated. Si ilikuwa mcheze na Club bingwa ya Morroco?
 
Kwani kuna sehemu nimesema hivyo. F.C. E. Ksaifa ndo nimeandika. Tukutane kwa machina maana kule hakuna kujitoa[emoji3]
Hatuna wasiwasi kukutana kwa mchina. Ndiyo siku mtaanza kusambaratika. Tayari mmeanza kusema katika imekiukwa. Mashamba ya mkonge ya Mo yanarudi serikalini.
 
Mkuu nipo sana tu.
Zamu yenu hii muitumie vyema.
Exactly mkuu..hii ni fursa yetu. Na Wewe kama hutaingia kwenye mabadiliko na ukategemea michango, yamkini itakuwa kama Ujerumani timu moja tu..!
 
Back
Top Bottom