Kutoka Uwanja wa Nangwanda Sijaona: Ndanda 1-2 Yanga

Kutoka Uwanja wa Nangwanda Sijaona: Ndanda 1-2 Yanga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Dk 1 Ndanda FC ndiyo wanaanza kushambulia kwa kasi

Dk 3, Ngassa anaachia mkwaju mkali, nusura afunge lakini hakuwa makini

Dk 4, Ngassa tena anaingia vizuri, anapiga shuti la chinichini, goal kick

GOOOOOOOO Dk 6, Buswita anafunga kwa ulaiiiini baada ya uzembe wa kipa na mabeki.

Dk 7, Ndanda wanapata kona, inachongwa hapa, Rostand anaokoa na kuwa kona tena

Dk 8, kona nyingi ya Ndanda, lakini Yanga wako makini wanaokoa hapa

Dk 10 shuti kali katika lango la Yanga, safari hii kipa yuko makini anaokoa, unamtoka anadaka tena

Dk 13, inaonekana kuna makosa mengi sana katika difensi ya Ndanda na wanapaswa kuwa makini

DK 15, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini mpira wa shuti la tik taka, unaishia mikononi mwa Rostande

Dk 18, Yanga inapata adhabu nje kidogo ya eneo la Ndanda

Dk 19, inachongwa faulo vizuri na Ajibu, inaokolewa vizuri

Dk 19, Ndanda wanapata kona, inachongwa lakini Yondani anaruka na kuokoa

Dk 20, Ajibu anaachia mkwaju matata kabisa lakini kipa anaokoa kwa umaridadi kabisa. Kona

Dk 20, kona maridadi ndani ya lango la Ndanda, kipa Kisubi, anatoka na kuupiga ngumi

Dk 23 nafasi nzuri nyingine kwa Yanga, kipa anaugusa, Ndanda wanaokoa

Dk 25 Yanga wanalazimika kumuweka chini Ngassa, lakini mpira faulo naye anapiga nyanya kabisa na Rostand kama maji anadaka

DK 28, pasi ya Buswita, Martin anajaribu lakini ni shuti mtoto

GOOOOOOOOO Dk 29 Kessy anachambua kama karanga kabla ya kuandika bao saaaafi la pili
Dk 32, Martib anaingia vizuri lakini anaanguka na kipa anauwahi mpira

Dk 34, Yanga wanachofanya ni kuupoza mpira wakisikilizia mabao yao mawili lakini wanashambulia kwa kushtukiza kila wanapopata nafasi

PENAAAAAAAAAAAAAAT Dk 36, Yanga wanapata penalti baada ya beki wa Zabron kuunawa

Dk 40, anakwenda kupiga Tshishimbi, kipa anadaka na kuuficha kabisa

SUB Dk 40 Waziri Majogoro anaingia kuchukua nafasi ta Baraka upande wa Ndanda

Dk 42, krosi nzuri ndani ya lango la Ndanda, Kisubi anatokea na kudaka vizuri kabisa hapa

Dk 44, Majogoro naye anaachia mkwaju hapa lakini hakulenga lango

Dk 45, Abdallah naye anaachia mkwaju lakini hakulenga lango

MAPUMZIKO
 
Yanga wameususa uzi Jana mida kama hii uzi wa simba ulifika page ya 11 sijui
 
Mpira wa Yanga unasikitisha,eti mwakilishi wetu kimataifa,mi nitoeni kabisa siwezi wakilishwa na timu bovu namna hii.unajiuliza yule ni kipa au koti?
 
TE="OKW BOBAN SUNZU, post: 25991399, member: 52569"]Nilikuwa na Malinzi tukioka viporo na marefa wetu[/QUOTE]
Zamu yako mwaka huu ule viporo.
 
Back
Top Bottom