Kutoka Uwanja wa Taifa: Kagera Sugar 1 - 0 Simba FC, Kagera watibua rekodi ya kutokufungwa ya Simba

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
MPIRA UMEKWISHA: Kagera Sugar wanatibua rekodi ya Simba kutofungwa mechi yoyote uwanja wa Taifa baada ya kuwashinda mabingwa hao wapya 2018 kwa 1-0. Utaratibu waandaliwa ili Rais Magufuli akabidhi Kombe kwa washindi

Kaseja kama kawaida yake amedaka penalti ya Okwi katika dakika za nyongeza.

Simba SC 0 - 1 Kagera Sugar
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Kagera Sugar, mechi ya Ligi Kuu Bara

1. Said Mohamed
2. Nicholas Gyan
3. Mohamed Hussein
4. James Kotei
5. Paul Bukaba
6. Erasto Nyoni
7. Shomary Kapombe
8. Jonas Mkude
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Shiza Kichuya

Kikosi cha akiba

12. Ally Salim
13. Salim Mbonde
14. Kelvin Faru
15. Mzamiru Yassin
16. Said Ndemla
17. Rashid Juma
18. Moses Kitandu

Rais Magufuli aliyehudhuria Uwanjani hii leo ametoa neno.

Rais Magufuli amesema Tanzania imechezewa siku nyingi tangu uhuru mwaka 1961 lakini timu zote za michezo hazijafika mahali ambapo ni patamu

- Amesema yeye haendi viwanjani kwa sababu ya 'frastruation' ya timu za Tanzania kushindwa hivi viongozi wa vyama vya michezo waweke mikakati kuondoa aibu

Rais Magufuli ameiomba Simba wakalete kombe la klabu bingwa barani Afrika kwani amewaheshimu kufika uwanjani .

-Amesema mpira walioonyesha leo mbele ya Kagera hawataweza kushinda kombe hilo
 
inakera sana!
simba badala ya kuweka record ya kutokufungwa hadi mwisho, Leo karuhusu bao kufungwa NA kagera sugar!
Wameharibu raha yooote! bora wangefungwa tangu mwanzo tukajua moja; walichokifanya Leo hakika ni sawa NA kutunza bikira usichana wooote halafu unabakwa siku ya kwenda kufunga ndoa; hata ndoa yenyewe haina radha tena! simba mmezinguaaaaaaa!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…