Kutokana na changamoto za maisha nimependela nifanye cha ziada ili niweze kukuza biashara yangu.

Kutokana na changamoto za maisha nimependela nifanye cha ziada ili niweze kukuza biashara yangu.

wrong turn

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
438
Reaction score
170
Habari wapendwa.

Naomba mchango wenu, kwa wale waungwana na wenye uelewa jinsi ya maisha yalivyo hivi sasa.

Ni kijana nilie jiajiri kwenye fani ya ufugaji wa kuku wa kisasa na kienyeji, nina diploma ya biashara.
Badala ya ufugaji, ningependa kukuza biashara yngu kwa kutengeneza vyakula vya mifugo hususan kuku wa kisasa, kutokana na changamoto ya upandaji bei wa vyakula kutoka kwenye makampuni ya vyakula vya kuku wa kisasa,nimeona nibora nitengeneze mwenyewe na ikibidi niuze, kwavile hapa kwtu tuna maligafi zakutosha ili niwez kufanya hivy, naomba elimu kutoka kwenu ili nifanikishe ndoto hii.
Mali gafi kuu nitakazo tumia kwa utengenezaji wa chakula kwa kuku wakisasa ni:-
- Mahindi.
- Soya.
- dagaa.
-alizeti.
Mali gafi hizi hutaka utaalamu wa kujua DCP ili ziweze kutoa mafanikio yaliyo na dhamna.

Tatizo langu ni hichi kipimo, kinapatikana hapa kwtu tz?, kama ndio kiko sehem gani, km sio naweza kukipata wapi?.
kwa vile mali gafi zote hizo tunazo hapa kwetu, jee kuna mtu anaweza kutoa ufafanuzi wa DCP ya maligafi hizo kulingana na mikoa zinako patikana?, kwa mfano soya, mahindi na nk ya mbea ina DCP...........

Naombeni mashirikiano yenu, wahitaji wa hiyo elim tuko wengi tunaomba mtupe elimu ili tujitegemee zaidi na kusaidia wengine.

Natanguliza SHUKURANI.
 
Back
Top Bottom