Kutokana na machinga kuuza bidhaa zinazolingana na za madukani, TRA watatenganishaje?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Kutokana na machinga kuuza bidhaa zenye ukubwa pengine na hadhi inayofanana na bidhaa za maduka yanayotoa risiti ambayo ndiyo kampeni ijayo, TRA watatofautishaje? Bidhaa hizi?

(Ipo haja ya kutengeneza machinga receipts)

#kwa ukweli machinga wanavuruga mfumo wa ukusanyaji kodi.

FB_IMG_16436129997692188.jpg
 
Mfanyabiashara atakuuzia vitu bila kukupa risiti atakuambia ukikutana na TRA waambie umenunua kwa machinga.

Ili kazi hiyo ifanikiwe TRA waunde task force kubwa ambao watajifanya ni wanunuaji wazunguke madukani kujifanya wananunua hapo watakamata wengi.
 
Kuwakamata haitasaidia chochote. Inabidi wawawekee mfumo maalumu wa kulipa kodi tofauti na ule wa cardi ya elf-20 “ kwa miaka yote, wawekewe utaratibu mzuri waishi maisha yao hii nchi sio ya wabunge peke yao
 
Neno hili Machinga linatumika Vibaya! Machinga ni yule anayeuza bidhaa zake akitembea mtaa kwa mtaa huku amezibeba, hawa wengine ni wafanyabiashara kama wengine, wapo wa chini, Kati na Juu, Ila Wanafanya biashara zao katika sehemu ambazo si rasmi
 
Ukishaona mfumo unatumia nguvu badala ya akili ujue kuna matatizo. Mm sijui tunafeli wapi kama nchi kudhibiti bidhaa na huduma mwanzoni mwa mzunguko kabla mlaji wa mwisho hajafikiwa.

Kama viwanda vyote vya uzalishaji na suppliers wakubwa wote wanaoingiza mzingo kutoka nje(Namaanisha mzunguko wa uuzaji unapoanzia) wakibanwa na system kwamba bidhaa zao zote ziwe zinajulikana na kuhakikisha kwamba kila anayenunua kwao anapewa risiti na kutozwa VAT baada ya hapo wasambazaji wanaofuata wote hawatakubali kulipishwa VAT, lazima watataka kuirudisha ile VAT na ili uirudishe lazima utoe risiti ili anayenunua ailipie yeye.

Kwann wafanyabiashara hawataki kutoa risiti? Jibu ni kwamba na wao wana bidhaa ambazo hazina risiti, hawakulipa VAT wakati wananunua mzigo. Sasa yule wa kwanza kabisa ndo akibanwa wengine watajikuta wako ndani ya mfumo maana asipotoa risiti wakati yeye alipewa risiti examination itamuumbua.

Kinyume na hapo ni staff tu wa TRA ndo watahongwa maisha yaendelee.
 
You have a point lakini....labda nitoe mfano, nimeingiza item X value 100/- vat 18/- tu. Nikaiuza 1000/- vat 160/-. Nikitoa risiti nitalipa tra 160-18 as vat 142/- nisipotoa risiti hio 142/- yote yangu.
 
Sasa ukiagiza item X, kama TRA itakuwa na mfumo wa kuhakikisha kuwa unapoagiza hiyo item x yako yote inakuwa registered ni rahisi sana kumonitor movement ya item x yako.

Ukiuza item x bila risiti siku wakikufanyia inspection au audit watajua maana watategemea kukuta item x ambayo ipo registerd na wewe utakuwa huna maana umeiuza.

Unapigwa faini kubwa sana maana umepoteza movement track ya item x kutoka kwako kwenda kwa mtumiaji wa mwisho na unalipa na hiyo VAT.

Ukitoa risiti uliyemuuzia item x kama anaenda kuuza tayari TRA itajua item x huna wewe anayo mtu uliyemuuzia, akiuza bila kutoa risiti na yeye imekula kwake maana atalazimika kudanganya kwenye hesabu kuwa anayo item x then atadakwa kwenye audit maana hana item x. Hivyo hivyo mpaka mtu wa mwisho.

Ukideal na registration ya mzigo unapoanzia, hawa wa katikati hawana ujanja, mfumo utawabana.

Hakuna haja ya kusumbua wananchi na kamata kamata deal na big fish wanaopeleka mizigo huku chini kwa watumiaji wa mwisho, shuka nao mpaka ukifika kwa wasambazaji wadogo wadogo unaachana nao maana wengi ni maduka madogo madogo yasiyo na VAT na machinga.
 
Sasa ukiagiza item X, kama TRA itakuwa na mfumo wa kuhakikisha kuwa unapoagiza stock yako yote inakuwa registered ni rahisi sana kumonitor movement ya mzigo wako.

Ukiuza bila risiti siku wakikufanyia inspection au audit watajua maana watategemea kukuta stock ambayo ipo registerd na utakuwa huna maana umeiuza.

Unapigwa faini kubwa sana maana umepoteza movement track ya stock kutoka kwako kwenda kwa mtumiaji wa mwisho na unalipa na hiyo VAT.

Ukitoa risiti uliyemuuzia kama anaenda kuuza tayari TRA itajua mzigo anao yeye, akiuza bila kutoa risiti na yeye imekula kwake maana atalazimika kudanganya kwenye hesabu kuwa hana hizo sales then stock itakuwa kubwa atadakwa kwenye examination. Hivyo hivyo mpaka mtu wa mwisho.

Ukideal na registration ya mzigo unapoanzia, hawa wa katikati hawana ujanja, mfumo utawabana.
Sio rahisi kihivyo.
 
Sio rahisi kihivyo.
Ndivyo inavyotakiwa kuwa. Siyo rahisi kwanini? Tuna njia mbili tu za kupata bidhaa humu nchini ambazo ni viwanda na kuagiza nje.

Unadeal na bulk suppliers tu, kadri mzigo unavyotoka kutoka kwa suppliers wakubwa unaenda na unagawanyika kwa suppliers wadogo, wakifikiwa wale ambao sio VAT registered unaacha. Kwann iwe ngumu?

Kwann iwe rahisi kusambaza watu mitaani kutegea wakati wa kupeana risiti halafu iwe ngumu kutengeneza mfumo wa stock registration?
 
Inahitajika workforce kubwa sana kwa jamii hii ya wasiopenda kulipa Kodi. Kulipa kwa hiari ndio Siri ya mafanikio ya wenzetu. Tufundishwe kuwa compliant tangu utotoni.
 
Mkuu, hakuna mtu asiyetaka faida kubwa, hata huko nje wanakamata sana wakwepa kodi na kuwafungulia mashtaka. Mfumo bora wa utambuzi ndio unaosaidia serikali kukusanya kodi nyingi. Shida ni kwamba sisi mfumo wetu upo vizuri kwenye makaratasi ila ukija kwenye uhalisia una leakage nyingi.

Mfano: Naagiza container la yeboyebo, likifika nikishalipa ushuru tu nawapa machinga. Hapo mm lazima nitakwepa kulipa VAT sababu machinga sio VAT registered, nikilipa VAT itaniumiza. Ila kama mfumo utanilazimisha kuwa lazima niulipie VAT nitabakiwa na option mbili tu, either nipandishe bei au nimuuzie mtu ambaye ni VAT registered.

Yaani ukishawaacha big fish wakakimbia na kodi, usitegemee hapa katikati utaipata hiyo kodi. Utatumia nguvu kubwa sana. Ndo hivi sasa na matangazo ya nyumba kwa nyumba kusaka risiti.
 
Mfanyabiashara atakuuzia vitu bila kukupa risiti atakuambia ukikutana na TRA waambie umenunua kwa machinga.

Ili kazi hiyo ifanikiwe TRA waunde task force kubwa ambao watajifanya ni wanunuaji wazunguke madukani kujifanya wananunua hapo watakamata wengi.
Hilo nalo ni la kuangalia
 
Mkuu, hakuna mtu asiyetaka faida kubwa, hata huko nje wanakamata sana wakwepa kodi na kuwafungulia mashtaka. Mfumo bora wa utambuzi ndio unaosaidia serikali kukusanya kodi nyingi. Shida ni kwamba sisi mfumo wetu upo vizuri kwenye makaratasi ila ukija kwenye uhalisia una leakage nyingi.

Mfano: Naagiza container la yeboyebo, likifika nikishalipa ushuru tu nawapa machinga. Hapo mm lazima nitakwepa kulipa VAT sababu machinga sio VAT registered, nikilipa VAT itaniumiza. Ila kama mfumo utanilazimisha kuwa lazima niulipie VAT nitabakiwa na option mbili tu, either nipandishe bei au nimuuzie mtu ambaye ni VAT registered.

Yaani ukishawaacha big fish wakakimbia na kodi, usitegemee hapa katikati utaipata hiyo kodi. Utatumia nguvu kubwa sana. Ndo hivi sasa na matangazo ya nyumba kwa nyumba kusaka risiti.
Umelielezea kiuchumi haswa,Safi sana
 
Machinga apaswi kulipa kodi sababu kodi ishalipwa bandarini au kiwandani kwann kuwepo kodi juu ya kodi
Mfumo wetu wa kodi hauruhusu hilo! Mbona makontena yanalipiwa mamilion lakini yanapofika madukani kodi zingine hufuata.
 
Mwenye uelewa kuhusu mfanyabiashara anayetakiwa kulipa kodi anatakiwa awe na mtaji au mapato kiasi gani, maana nchi za wenzetu watu wenye biashara ndogo ndogo ambazo hazijafika mtaji kiasi fulani au mauzo na faida kiasi fulani wapo exempted kwenye kulipa kodi. Mwenye uelewa hapa kwetu tunaomba atujuze ni biashara ya ukubwa upi inayoanza kutozwa kodi.............
 
Mfumo wetu wa kodi hauruhusu hilo! Mbona makontena yanalipiwa mamilion lakini yanapofika madukani kodi zingine hufuata.
Bidhaa moja ulipiwa kodi mara sita chukulia mfano mazao Mchele au unga utalipa kodi ukianza kulima,kupanda,kuvuna, kusafirisha sokoni, kupeleka kiwandani, utalipa kodi kiwandani, ukisafirisha kurudi sokoni, dukani, nk
 
Back
Top Bottom