RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,788
- 4,401
Taarifa ya CAG ilionekana kukera viongozi wa juu wa serikali na nilijuwa kuwa hatua kali kwa wabadhilifu hadi sasa wangekuwa hawapo maofisini kumbe kilikuwa kiini macho cha kuonesha chukizo mbele ya umma huku vitendo hamna katika uwajibikaji.
Nachofikri ni kwamba kama mama ataongoza serikali hii hadi 2030 kwa mtindo huu watu wa chini watapata taabu sana maana huduma za kijamii nyingi zitazorota kwa kuwa kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake, Ni vigumu sana kuelewa nachosema hasa kwa watu ambao wanapata asali mojakwamoja ndani ya serikali hawa watu wamejaa matusi na kejeli hadi imefikia hatua wengine wanatembea na kusema " usipopiga hela ya serikali sahivi nakufanya maendeleo utakuwa mjinga " maneno hayo yanafikrisha sana .
Mimi nimalize kwa kusema mama awe makini anaweza kukamilisha baadhi ya miradi lakini ikawa haina ubora kutokana na usimamizi mbovu nyote mnajuwa ubovu wa baadhi ya vitu tumejionea kuletewa mabehewa ya mitumba huku uwezo wa kununua ulikuwepo ; mambo haya kwanini yafanyike waziwazi? wengine wanasema mama kwa baraza alilonalo hana mtu wa kumkoromea maana anawaona kama ndiyo injini zake katika uchaguzi ujao,
Pili kutokana na taarifa za siri zilizopo yule mzee wa msoga inasemekana ndiye anayempa ushauri wa kila kitu jambo ambalo mama hata vijana wa msoga wakiharibu anashindwa kuwaajibisha . ndugu zangu ma bibi na mabwana kwa sasa tufunge mikanda kama unajuwa haupo kwenye mfumo utapiga kelele kama hizi mwisho wa siku hata watu wasiojulikana ukizidi kelele watapita na wewe.
Nachojuwa mungu yupo dua zetu zinaonekana hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, tunashukru mungu kwa kila jambo!
jioni njema.