Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakuu naomba kukiri kwamba mimi si mtaalam wa sheria za Tanzania , hivyo uzi wangu waweza kuwa na mapungufu kadhaa , lakini ni dhahiri kwamba kwenye nchi hii sheria za uchaguzi zinawataka wagombea kudhaminiwa na chama cha siasa , kwa maana kwamba ili uweze kukubaliwa na Tume ya uchaguzi kuwa mgombea wa ubunge , udiwani ama Urais unapaswa kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa na Msajili wa vyama vya siasa .
Na kwamba ikiwa utavuliwa uanachama na chama hicho ama wewe binafsi kujivua uanachama basi bila shaka utakuwa umepoteza Ubunge wako na kutotambuliwa kama mbunge .
Cecil Mwambe tunataarifiwa kwamba amerejea bungeni ambako yeye mwenyewe aliondoka baada ya kujivua uanachama wa chama kilichomdhamini baada ya kumuokota barabarani 2015 na kumpa nafasi ya kugombea ubunge wa Ndanda baada ya kutupwa na ccm , na amerejea kwa hisani ya Spika wa bunge hilo Mtukufu Ndugai , kwa kadri ya ufahamu wangu huku ni sawa na kudharau na kusigina kabisa katiba ya nchi , yawezekana mimi labda sielewi , naomba wanasheria mnisaidie , na ikiwa kama spika wa bunge anaamua kunyea katiba ya nchi mnadhani kuna haja ya raia wa kawaida kuiheshimu ?
Nakala : Tundu Lissu