Asante kiongozi .Nchi yetu ilianzisha bodi ya mfuko wa barabara yani “LOAD FUND”
Bodi ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa SHERIA YA BARABARA NA TOZO YA MAFUTA, SURA YA 220. Bodi hii inaundwa na wajumbe tisa, wanne kutoka sekta ya Umma na watano kutoka sekta binafsi.
Wajumbe hao ni Mwenyekiti (kutoka sekta binafsi), Katibu Mkuu - Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu - Wizara ya Fedha na Mipango, Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Mwakilishi wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania, Mwakilishi wa kutoka Hifadhi za Taifa - Tanzania, Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania na Mwakilishi kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania.
Tunaona mafanikio makubwa katika mfuko huu kwani barabara nyingi zimekuwa zikijengwa chini yake na imetekeleza miradi mbalimbali hivyo basi kuundwa kwa Bodi ya mfuko wa ajira kutoka katika vyanzo vya kodi mbalimbali kutawezesha kupatika kwa fedha za kuajiri ajira mpya na kuongezeka kwa mishahara kwa wafanyakazi ni hayo tu kiongozi