Kutokuvaa soksi siyo uhuni!

Kutokuvaa soksi siyo uhuni!

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Wa- mbulu na wa-Iraqi wote ni ndugu!

Wakuu kumekuwa na kasumba ya kwamba,kila unapovaa kiatu ni lazima uvae soksi!

Binafsi soksi nilivaa wakati nikiwa shule kwasababu ilikuwa ni lazima kwakuwa ilikuwa ni moja ya sare za shule!

Juzi moja nimeenda mahali fulani nikiwa nimekula suti (Kaunda suti ) ya mikono mirefu halafu chini sikuvaa soksi Bali nilipiga moka yangu safi nikawa nadunda kama kitenesi!,Kwakuwa Nina cheo mahali fulani !,nikawa nasikia maneno kutoka Kwa watu wangu wa karibu ya kwamba,eti wanazungumza kwamba kiongozi asiyevaa soksi ni Muhuni na hapaswi kuaminiwa!

Niliwashangaa sana watu wanaozungumza hivyo kwasababu wao yawezekana ndiyo wakawa na matatizo!

SABABU ZA WATU WENGI KUVAA SOKSI

1.Kama Urembo au utanashati!

2.Kubana vizuri mguu ndani ya kiatu!

Binafsi huwa nilivaa soksi nashindwa Kutembea vizuri kwasababu kiatu kinakuwa kama kinateleza!

Pia nikivaa soksi nakuwa nakosa uhuru wa kujiachia,!

Mwisho,naona kama kuvaa soksi ni Ushamba!

Kama mtaendelea kuniona Muhuni endeleeni kuniona Muhuni but siwezi kuvaa soksi kwasababu zinanikosesha uhuru!
 
Juzi moja nimeenda mahali fulani nikiwa nimekula suti (Kaunda suti ) ya mikono mirefu halafu chini sikuvaa soksi Bali nilipiga moka yangu safi nikawa nadunda kama kitenesi!,Kwakuwa Nina cheo mahali fulani !,nikawa nasikia maneno kutoka Kwa watu wangu wa karibu ya kwamba,eti wanazungumza kwamba kiongozi asiyevaa soksi ni Muhuni na hapaswi kuaminiwa!
Ni uhuni kwa mujibu wa kitabu gani
 
Sijasoma sana ila usijitetee, Unapovaa Official hasa suruali yako isiwe ndefu vya kutosha hakikisha unavaa Socks.
Kweli si uhuni ila ni ubishoo wa kitoto sana.

Moka na kitambaa bila socks ni Ushalobalo sawa kabisa na kuvaa Katakei.
 
Katika vitu sina time navyo ni soksi na mkanda.
Wewe ni kama Mimi mkuu!
Hizi ni akili za kitoto zimekutana, Mnaleta mambo ya Uniqueness na Ushalobalo kwenye vitu serious, Muwe mnavaa hivi mkienda kupiga picha, kuparty na marafiki au sehem zingine zote zisizo na sheria.

Kazini, Kanisani, Ukweni nk acha hizi tabia unajidhalilisha inaonyesha kiasi gani bado unasumbuliwa na "Uvulana" na kama ni mzee basi ndo wale tunasema "Hakui"

Siko mbali na nyie napenda kuvaa Causal lakini huwa nazingatia mazingira ili kulinda heshima yangu mbele ya Watu wazima, viongozi na wengine wote wanaoamini katika uvaaji huu vijana tunaouna mzigo.
 
Hizi ni akili za kitoto zimekutana, Mnaleta mambo ya Uniqueness na Ushalobalo kwenye vitu serious, Muwe mnavaa hivi mkienda kupiga picha, kuparty na marafiki au sehem zingine zote zisizo na sheria...
Kazi ya Soksi kwenye kiatu ni ipi hasa?
Je ,kazi ya mkanda ni ipi hasa?

Yawezekana wewe ndiye ukawa na tatizo la kiakili!

Ninachojua sifanyi dhambi Kwa kutokuvaa vitu hivyo,tofauti na hapo kama watu wanaongea ngoja waongee!
 
Siyo sawa mkuu,kutokuvaa soksi siyo ubishoo!
Nimekushauri tu, kama umevaa Jeans na Raba hapa kuvaa socks ni Afya tu si lazima maana haya si mavazi ya kazini hivyo utakua zako mtaani ila unapovaa Oficial Moka na Cardet au Kitambaa socks ni Sheria vinginevyo huu ni Ushalobalo wa Kitoto na inaonyesha wazi lengo lako si kazi ni attention.
 
Kazi ya Soksi kwenye kiatu ni ipi hasa?
Je ,kazi ya mkanda ni ipi hasa?

Yawezekana wewe ndiye ukawa na tatizo la kiakili!

Ninachojua sifanyi dhambi Kwa kutokuvaa vitu hivyo,tofauti na hapo kama watu wanaongea ngoja waongee!
Basi kesho nenda kazini kwako na Pensi na Kobazi, Tshirt na Kofia.
Kuna standards zimesetiwa ili kulinda hadhi ya Office na kudumisha ustaarabu wa wafanyakazi

Si mara zote utavaa ili upendeze au ujisikie fahari vile unapenda wewe.

Ukianza kuona Sheria ni mzigo au Ushamba basi ujue unashida kichwani.
 
Back
Top Bottom