SoC02 Kutokuwa na haki na usawa katika elimu, sehemu za kazi, ndani ya nchi na baina ya nchi na nchi

SoC02 Kutokuwa na haki na usawa katika elimu, sehemu za kazi, ndani ya nchi na baina ya nchi na nchi

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 30, 2022
Posts
28
Reaction score
24
Kutokuwa na haki na usawa ndio mwanzo wa matatizo yote tulionayo, iwe vita, iwe umaskini au uongozi mbovu yote yanasababishwa kutokuwa na haki pamoja na usawa.

Na bila kujenga haki na usawa hata tufanye kazi usiku na mchana kama akuna haki kwenye maslahi bado watu watazidi kuwa maskini , au hata tuwe na viongozi wazuri kama sheria zetu hazina usawa katika mihimili yake watashindwa kuongoza vizuri.

Kwa jina naitwa Prince Ndeserua ni mhitumu wa Stashahada ya ukadiriaji majenzi, naishi kujijenga katika misingi ya falsafa.

Twende pamoja katika haki na usawa ambao wengi hatufahamu kama ni tatizo na njia zake za kutatua.


》KUTOKUWA NA USAWA KWENYE ELIMU.
Utofauti wa lugha mashuleni baina ya shule binafsi na za serekali tunachukulia tu kirahisi. Labda ungekuwa wa kijinsia yani wasichana wajifunze kutumia kiswahili, na wavulana watumie kingereza kwa muda miaka saba alafu kuendelea wote watumie lugha ya kingereza hapo labda tungepaza sauti kwa vile inamhusu mtoto wa mkulima wa chini nani atapaza sauti.


NINI KIFANYIKE:
Kwanza tutambue utofauti wa lugha mashuleni ni ubaguzi kama ulivyo ubaguzi mwengine kama vike wa kijinsia.

Serikali inapaswa kutumia lugha moja kufundishia au itumie lugha mbili hadi mwisho (sekondari hadi vyuo vikuu) na kuwe kuna fursa sawa ila sio lugha tofauti alafu zinaishia njiani ni kumiza watu wengine.


》 KUTOKUWA NA USAWA KWENYE MASLAHI YA KAZI.

Watu wengi wanafanya bila kuwa na mikataba na pia wanacholipwa ni kidogo sana akijitoshelezi.
Dhuluma ya malipo ya malipo wafanyakazi aimuathiri tu mfanyakazi tu bali ni jamii nzima.

Kwa sababu huyo mfanyakazi atashindwa kufanya manunuzi na pia kodi atalipa kidogo au atolipa kabisa.

Na hi ndio sababu nchi kipato kinaongezeka viwanda makampuni kila kitu kinakuwa ila maisha ya watu wanazidi kuwa duni.

Kwa hiyo mfanyakazi akidhulumiwa ni jamii nzima imedhulumiwa biashara zitashindwa kukua, kodi serikali itakosa pia hao ndio wawezaji kwenye binafsi hivyo sekta binafsi zitapungua au zinashindwa kukua vizuri.

NINI KIFANYIKE:

Watu wote tujue jukumu la kupambana maslahi ya wafanyakazi ni la kwetu sote kwani madhara yake sio kwa mfanyakazi bali jamii nzima.

Bila hivyo viwanda vitakuwa , kampuni na kipato cha nchi ila wary wengi watazidi kuwa maskini kama akuna usawa wa kimaslahi.

Takwimu zote za wafanyakazi isiwe tu idadi iwe zinasema na wastani wa mishahara yao au kipato chao kujua wapi kuna shida.

Pia tasisi za wafanyakazi ziwe mamlaka ya kujua kila mfanyakazi analipwa shilingi ngapi na wakati gani kila mshara anavyopata wapate taarifa maana ni ngumu mfanyakazi kuripoti kwao kwani inajenga uhasama kazini kwake.

》 KUTOKUWA NA USAWA NDANI YA NCHI.

Akuna usawa baina ya mihimili ya kiserekali kuanzia mhimili wa bunge yani wakilishi wanakuwa mawaziri na manaibu hadi waziri mkuu alafu bado ni wawakilishi wetu bungeni ndio hao wameemda kuwa serekali. Na pia Raisi kuteuwa majaji kunafanya nchi kuongozwa na mhimili mmoja tu.

NINI KIFANYIKE:

Inahitajika katiba mpya ambayo itaipa mamlaka sawa mihimili yote na kufanya ijitegemee.

》 KUTOKUWA NA USAWA BAINA YA NCHI KWA NCHI.

Siku zote tunaishi tunaona mataifa makubwa yanatawala mataifa mengine kwa kila nyanja uchumi, kisiasa na kiutawala.

Kama vike vikwazo vya uchumi au hata uvamizi wa moja kwa moja kama vile uliopo wa Rusia dhidi ya Ukraine.

Hakuna amani hata kama amna vita silaha kama nyuklia au viongozi wa mdikteta wenye nguvu ukimwenguni imekuwa tishio katika dunia ya sasa hivi maana maamuzi yao yanaigharimu dunia nzima.

NINI KIFANYIKE:

Kuungana kuwa na jeshi la pamoja la dunia itakuwa suluhisho la kudumu kutakuwa hakuna mkubwa wala mdogo, wote tutakuwa sawa.

Bila hivyo ni ngumu sana tuona UN licha ya kuwa sheria zote nchi nyingi hazitekelezi kama vile kuzuia silaha za nyuklia ama nchi kuvamia nchi nyengine ata uhuru wa demokrasia aufuatwi.


HITIMISHO
TUNAISHI KATIKA DUNIA INATATIZO KUBWA MBAYA ZAIDI ATUJUI KAMA TUNATATIZO TUNAONA TUKO SAWA ILA ATUKO SAWA HATA KIDOGO.

NAAMINI TUNATEMBEA NA KIATU KIMOJA MGUUNI HASA ULE AMBAO NI DHAIFU SIKU ZOTE UNATEMBEA PEKU AUNA HAKI HATA KIDOGO.

NI SAWA NA HII PICHA INAONYESHA TUMEVAA SHUKA YANI TUMELALA LICHA YA KUWA NA KIATU KIMOJA TU MGUUNI KUTOKUWA NA USAWA JAPO KUWA KUNA KISU MGUUNI KUONYESHA MAUMIVU ILA BADO TUMELALA.


FB_IMG_1661876796831.jpg
 
Upvote 1
Mkuu naona umeweka na kapicha.......uko juu...lol,

Nimependa topic yako, serikali ichague lugha moja ya kufundishia...i guess kwa vile bado tunahitaji kuingiliana na mataifa mengine lugha hio iwe Kiingereza. It makes me sad kuona tunawagawa wanafunzi kwa kutowapa lugha ya Kiingereza watoto wanaotoka familia zenye kipato duni.

Kufundisha shule za serikali Kiingereza mpaka watoto wajue lugha hio ni jambo linalowezekana, serikali haijaamua kuwekeza/kuinvest kwenye jambo hilo tu. Tunajenga matabaka ya kijinga kwamba wachache wapate a better start.

Hio ya pili ya kujenga usawa kwenye maslahi ya kazi, unapoteza muda ndugu..ni mpaka hapo uchumi uimarike na watu wawe na elimu, na CCM haitaki watu waelimike wajue haki zao....ukitaka usawa CCM must go!
 
Asante sana Anita, S
Picha imebeba ujumbe mzima.
Tunapmbana kila siku kutafuta suluhu ya matatizo yetu mengi tulionayo tunashindwa kuyatatua kwa sababu kuu tunasahahu yamesababishwa kutokuwa na haki na usawa na atushuhuriki nalo.

Suala hasa kupigania maslahi ni jukumu la jamii nzima kama tukitaka tuondokane na umaskini na utofauti wa kipato (income inequality) kama tukitaka kila mtu aishi vizuri lazima kuwe na usawa wa kimaslahi.

Siku zote mwenye hela atazidi kunyonya maskini mpaka pale jamii ikiamka na kupigania haki zao bila hivyo hao wafanyakazi ndio tunaishi nao kwmeye jamii ikiwa awana hela watashindwa kuwekeza katika jamii au kufungua biasha maana sekta binafsi zitashindwa kukua hata pia watumiaji yani wanunuzi.

Watu wengi sana saivi kutokana na shida ya ajira wanalipwa kidogo sana kama mtu anastahili kulipwa laki nane au milioni akilipwa laki mbili au tatu manisha jamii imekosa hiyo hela siyo yeyr peke yake.

Mfano mzuri Tanzania tuna migodi mikubwa Afrika Geita ni wapili kwa sasa kiukibwa ukiangalia migodi mingi Africa kama Ghana, Saudi Arabia, Egypt, Mali ata Congo au nje ya bara madini thamamni yake ile ile.

Wafanyakazi wao wanalipwa ukibadilisha na hela Tz kama milion sita hadi kumi na sisi sote tunachimba madini kwanini sisi tuwe source ya cheap labour iweje kwetu range iwe chini karibu mara kumi tano laki saba au nane au hata tano mpka milion.

Sisi tunachimba chuma au mawe tunaishia kuwafadisha wawekezaji wenyewe tu akifaaskini hata viwanda vinavyofunguliawa au makampuni kama akuna maslahi akuna faida jamii inapata.

Imagine wafanyakazi wetu wa migodini wangekuwa wanalipwa viziri jinsi gani maisha yangekuwa vuzuri mitaaani na sekta.

UWEZI UKAJENGA MAISHA BORA BILA KUWA NA USAWA WA KIMASLAHAI WATU WATAFANYA KAZI USIKU NA MCHANA WATAISHIA KUFA MASKINI KAMA TUSIPOGIGANIA HAKI NA USAWA KATIKA MASLAHI.

Tafadhali naomba niasidie lushare ujumbe ili tuzidi kuamka tupiganie haki na usawa.
Uwe na afya njema na siku njema.
 
Back
Top Bottom