Kutokuwa na hamu ya mapenzi kabisa! Hili ni tatizo?

Hidden Id

Member
Joined
Oct 11, 2018
Posts
26
Reaction score
25
Habari wanajukwaa!?

Kwanza naomba niwaombe radhi kwa kuja na ID mpya ingawa humu mimi si mgemi kwn hadi sasa nina miaka 8 ya uanachama.

Turudi katika mada!
Historia kwa kifupi
Kwa jinsia mimi ni mwanaume wa miaka 35 nina mke na watoto wawili ambapo hadi ss ndoa yetu inaelekea kuanza mwaka wa saba. Hatujawahi kuwa na malumbano wala kugombana na mke wangu, hivyo sina wala yeye hana tatizo lolote ktk mahusiano yetu.

Tukirudi nyuma kdg kiukweli nilikuwa napenda mapenzi sana kufanya na mke wangu japo mara moja (atleast game 2) karibu kila siku kwa miaka zaidi ya minne ambapo ilifikia mke wangu kuniomba mipunguze kasi au nioe mke wa pili kwani kwa dini yetu yaruhusu. (Kwa sisi watu wa Pwani hili la mke kukwambia kuoa sio geni sana). Nilijitahidi kupunguza kwa kujibidiisha na mazoezi na hatimaye ikawa naona kawaida tu kwa wiki mara 3 hadi 5 tunafanya. Hivyo sikuoa.

Kikazi nafanya kazi zinazohusiana na mahesabu! Mwanzoni mwa mwaka huu kuna nafasi nilipandishwa hivyo kupelekea "volume" ya kazi kuongezeka sana. Na ili kufikia target imenibidi kujiongeza hadi kufanya kazi nyumbani usiku katika ya saa 7 hadi 9 usiku (saa kiswahili). Mwanzo nilikuwa napata taabu, lkn kwa sasa nimezoea kiasi ht km sina kazi ikifika muda huu nakuwa macho sina hata chembe ya usingizi. Hili limedumu hadi ss inaweza kuwa imefika zaidi ya miezi 6.

Lkn nimekuja kunote jambo au tabia mpya kabisa kwangu. Yaani sina hamu kabisaaaa kabisaaa ya mapenzi. Sina hata chembe. Na hali hii huu ni mwezi wa nne hv. Mwanzo nilidhani labda naumwa nikafanya check up ya mwili wote sikuwa na tatizo, nikawa nahisi labda mgongo na misuli inauma ndiyo maana sina hamu coz mazoezi nimepunguza sana, hivyo nikaenda sehemu moja hivi ceragem center kupata tiba mazoezi nk lkn wala hata sishtuki. Asubuhi naamka salama na kawaida kabisa "mashine imesimama imara"! Lkn ile hamu ya mapenzi sina.

Ukija upande wa marafiki, ukweli mm sina maana wengi wanakuwa wananiuliza mambo yanayohusisha kazi ss hili linanikera sana kwn najikuta muda wote nawaza au nafanya kujibu maswali yanayohusiana na kazi tu. Kazi ni nzuri na naimudu vema sana na namshukuru Mola inalipa sana lkn inataka muda mwingi sana.

Je hali hii ya kutojisikia hamu ya mapenzi, inaweza kuwa ni ugonjwa gani? Au nimeathirika afya ya akili? Au nini hasa kinasababisha kuwa na hali hii? Naomba msaada wenu plz wataalam!
 
Pole mkuu,hali kama hii ilishanipata kipindi flan,nilikua napenda mapenzi sana,lkn mwanzo mke wangu alikua anaonesha ushirikiano lkn baada ya kujifungua na mtoto akakua nilianza kutengwa,kwa mwezi naweza kukutana nae kimwili mara 2 au 3,ilinipa shida sana kuzoea hali ile,nilichepuka siku moja ili kutuliza maumivu lkn nilijutia sana maamuzi yale,kwani nilitumia pesa nyingi bila sababu,dada alikua anaonekana mzuri high class kumbe wa ovyo hakuna analo jua,anamtambo kweli kweli pipa sio pipa

Kutokea pale nikachukia michepuko milele ikabidi nitulie tu nivumilie mateso,nilichokifanya ni kujiweka busy na mambo yangu ili angalau kupunguza ashki za mapenzi,nilifanikiwa kwa kiasi flan kutuliza so hata wife nikawa simsumbui kabisa,nami nikajikuta nakosa hamu ya mapenzi kabisa,siku akijisikia yeye ndo anaomba lkn mimi nilijiwekea siwezi kuomba ili nicop situation,baadae ikawa ugonvi tena mara nw days simsumbui nishapata michepuko mingine inayonipa,so tabu ikawa juu ya tabu nyumba haikaliki,kila siku kelele, kutokana na vituko vyake nimejikuta sipendi kabisa mapenzi,nishamrusu akitaka kuchepuka aende anakojua siwezi kupoteza muda kwenye upumbavu aliosababisha yeye,so pole sana bro mimi naona ni hali ya kawaida
 
tatizo kazi na kuchelewa kulala, kama kazi ni nyingi, fanya hivi, uwe unawahi kulala halafu unawahi kuamka hata saa9 usiku, bapo utapiga kazi na nanihii utakula.

Pia msosi, ulaji mbovu, watu wanagharamia vyakula na vinywaji ambavyo wala havina faida kiafya zaidi ni kuharibu afya ikiwa ni pamoja na kupoteza hamu. Mafuta mafuta mkuu punguza. Kula viti natural.

Tatu, michepuko, mkuu yani akili za wanaume wote huwa ziko hivi, ukiwa na mpenzi, ikitokea asioneshe kukuhitaji sana, siku akiyokea mwanamke mwingine ambaye anaonesha kukuhitaji either kwa muda wako, pesa, au mapenzi huwa mapenzi kwa mpenzi wako yanapungua, maana hakuna cha pekee unachokikosa kwake ikiwa unauwezo wa kukipata mahali pengine.

mawazo, rudisha fikra nyuma, kumbuka huyo ni mkeo, mpende kwa vyovyote, una thamani yake, taratibu hisia zitarudi tu.

Mengine wakushauri wenye ndoa wenzako
 
Anamtambo kweli kweli pipa siyo pipa, nimeinoti mkuu!
 
Asante Mkuu ISLETS

1. Kurudi nyumbani
Ratiba yangu ya kurudi nyumbani ni mapema tu muda wa kawaida haizidi saa 7:30pm hii inatokana na nikitoka kazini napita masjid hasa ile maghrib halafu narudi nyumbani wala sina kijiwe cha kukaa

2. Kulala
Ratiba yangu kulala hii toka nasoma haizidi saa 10:00pm haijawahi badilika, ila mabadiliko yamekuja ktk kuamka usiku wa manane hadi saa 3am

3. Vyakula
Vyakula navyokula kawaida sana. Mm sio mpenzi wa chipsi. Vyakula navyopenda si vya mafuta sana. Na vlvl kuruka kamba najitahidi sana kuondoa mafuta. Nilishaacha kunywa kahawa na chai nakunywa ya majani kdg sana

4. Mchepuko
Namshukuru Mwenyezi Mungu, sina ishu hizi kabisa. Nimejitahidi na najitahidi kuwa muadilifu kwa wife. Na vlvl ishu za kazi zinanifanya niwe ktk "cycle" fulani hv ambayo ni ya home------ibadani------kazini jp ktk mambo ya kijamii kama misiba, shughuli za jamii na hata sokoni hushiriki kwenda
 
Pole sana mkuu fanya mazoezi kunywa maji mengi kula matunda sana punguza vyakula vya mafuta kula samaki.
 
Asante sana Mkuu. Kuna jamaa alinicheki nae kanishauri nianze kunywa uji wa lishe uliotengenezwa home na km ikibidi nipate likizo na vlvl nimwone mtu wa saikolojia. Anasema nae ilimtokea akapewa ushauri huo ilimsaidia sana! Now yupo poa.
Pole sana mkuu fanya mazoezi kunywa maji mengi kula matunda sana punguza vyakula vya mafuta kula samaki.
 
Asante sana Mkuu. Kuna jamaa alinicheki nae kanishauri nianze kunywa uji wa lishe uliotengenezwa home na km ikibidi nipate likizo na vlvl nimwone mtu wa saikolojia. Anasema nae ilimtokea akapewa ushauri huo ilimsaidia sana! Now yupo poa.
Yap fanya hivyo pia hawa Mademu/wake zetu kwa maneno yao yanachangia sana kuloose hamu ya tendo...mcheck mwanasaikolojia pia.
 
Mashaallah jitahid Al akkhy huo muda unaoamka usiku uwe una swali walau rakaa mbili za Tahajjudu Allah akufanyie wepesi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…