Kutokwa maziwa kipindi cha ujauzito husababishwa na nini?

Nyanda lunduma

Senior Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
187
Reaction score
68
Habari za Leo wana JF.
Niende moja kwa moja kwenye maada hapo juu,Nina mpenzi wangu ambaye ana ujauzito wa miezi mitano kwa sasa , ila usiku akilala Maziwa huwa yanatoka wakati mwingine hata akiwa amekaa huwa yanatoka.
Naombeni mnieleweshe nini tatizo lake na nifanye nini niweze kumsaidia zaidi.

Naombeni msaada wanu wana Jf.
 
Tatizo wapi mkubwa hapo mwili unapitia mabadiliko mengi na makubwa sana kujiandaa na zoezi la kuleta kiumbe kipya.

Sasa ni wakati muafaka wa wewe kuacha kumnyonya mwenzako, subiria zamu yako.
 
Maziwa yanatoka sana ;amejaribu kuwauliza ambao tayari wana watoto wengi wanasema hiyo hali hawajapitia sasa mimi kwangu naona kama ni Tatizo.
Asante sana mkuu
 
Haya mambo yanatofautiana kati ya mtu na mtu. Inaweza isiwe tatizo ila kwa kuwa waliowengi hawajapitia hiyo hali, wasiwasi lazima uwepo.

Ameshatoa taarifa anapohudhuria clinic?
 
Mabadiliko ya kimwili usiwe na wasi, kuwa makini unapoenda nae clinic wasije kumpa dawa zikamzudhuru wakati atakapokuwa na mtoto, namaanisha zikaja kumsababishia mtoto kutokupata maziwa ya mamayake
 
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom