Naisweet inawezekana una ugonjwa unaoitwa endometriosis. Yaani kunakuwa na seli zinazofanana na za kifuko cha uzazi katika sehemu nyingine za mwili hasahasa tumboni. Seli hizi huwa zina tabia kama ya kifuko cha uzazi ndio maana zinaleta maumivu kipindi cha hedhi. Vilevile zinaweza kusababisha mtu kushindwa kubeba mimba.
Unfortunately matibabu yake ni kufanya operation kuona kama tatizo lipo na kuliondoa.
Je, umeshawahi kufanyiwa ultrasound? Imeonyesha nini?
Endometriosis haionekani kwenye ultrosound lakini ikiwa ultrasound iko normal na matatizo yanaendelea then inabidi kurule out hiyo.
Ushauri ninaoweza kukupa kwa sasa ni kutumia dawa za uzazi wa mpango ili kuirekebisha hedhi yako. Kutokana na jinsi mwili utakavyorespond kwa dawa hizo ndio daktari anaweza kupanga mikakati zaidi. Kwahiyo ni muhimu kuonana na gynecologist.