SoC04 Kutolewa kwa mitihani ya maandishi na kuanza kufanya mitihani kwa njia ya vitendo katika ngazi za vyuo vikuu nchini

SoC04 Kutolewa kwa mitihani ya maandishi na kuanza kufanya mitihani kwa njia ya vitendo katika ngazi za vyuo vikuu nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

ALLEN XSAVERY

New Member
Joined
Jan 29, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Vyuo VIKUU nchini Tanzania vilianzishwa baada ya uhuru wa Tanganyika mnamo mwaka 1961 .chuo Cha kwanza ,kuasisiwa mwaka 1970.

Tangu wakati huo hadi sasa serikali imekuwa ikiweka msisitizo mkubwa katika ujenzi na maboresho vyuo inavyotarajiwa kuendeleza taifa hili kwa kuongeza wasomi na wenye uweledi katika sekta mbalimbali nchini.

Je ni zipi sababu za msingi ya kuzuia MITIHANI ya MAANDISHI na KUANZA KUFANYA MITIHANI ya VITENDO ?
Kufuta mitihani ya maandishi na kufanya mitihani ya vitendo vyuo vikuu kunawezaleta faida kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

1. Kuimarisha ujuzi wa vitendo: Mitihani ya vitendo inawezesha wanafunzi kutumia maarifa yao katika mazingira halisi au karibu kabisa, hivyo kuwajengea stadi za utekelezaji. Hii inaendelea kufanyika katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo Norway katika sekta ya uvuvi wa samaki na viwanda vya samaki , Sweden pia pamoja na marekani .

1719054221912.png

Picha chanzo .Indonesia uvuvi wa data.

2. Kukuza uelewa thabiti: Wanafunzi watapata fursa zaidi ya kutumia ufahamu wao katika matatizo halisi au shughuli nyinginezo zenye umuhimu mkubwa. Na pia kuweza kutatua changamoto nyingi za hapa nchini ikiwemo migogoro pamoja na ukosefu wa ajira nchini

3. Kuboresha ustadi wa kitaaluma: Mitihani hiyo itasaidia wanafunzi kukua kiakademia kwakuwezesha kupima uelewaukamilifuuwanadamada kuliko mtindo wa maswaliiyanayohitaji majibumoja moja ambayo huwenda mwanafunzi kakariri Ili mradi akajibu mtihani huo ulio katika maelezo lakin kwa NJIA ya VITENDO itamrahisishia kukua kimaarifa

4. Kupunguza udanganyifu :Mitiani hiyo kwa NJIA ya VITENDO itasaidia kupunguza udanganyifu ambao u akuwa unatokea kwa vyumba vya MITIHANI kabla na baada ivo basi kufanya kwa Vitendo itakuwa NJIA nyepesi ya udanganyifu kupungua kwani muhusika mwenyewe atasoma kwa ufasaha Ili kufanya kwa Vitendo kwa usahihi .

1719053749941.png

Chanzo, baraza la MITIHANI Tanzania

5. Itaboresha uwiano mzuri kati ya mwanafunzi na mwanafunzi :kwa sababu uhusiano kati ya mwanafunzi na mwanafunzi utaonekana katika Vitendo hualisia katika sekta husika kwa mfano katika sekta ya usafirishaji upakuzi wa bidhaa katika bandari inavyofanywa kwa Vitendo ndiyo NJIA nyepesi ya kumchunguza mwanafunzi kama alielewa jinsi ya kupakia na kupakia MZIGO .

7. Kuongeza utashi: pia ufanyaji MITIHANI KWA Vitendo inaongeza utashi kwa mwanafunzi kwani kutapelekea kujiamini katika sekta ambayo atakuwa anafanyia kazi kwa wakati huo , na sio tu anapiga yia kazi inaweza kuwa msaada katika sekta nyingine kwa kuchangia mawazo na ubunifu alionao katika sekta nyingine

8. Pia itasaidia kukuza unadharia wa Vitendo katika viwanda ambavyo vinakuwa na kuongezeka nchini kwa sababu ya sayansi na teknolojia inayozidi kukua kila siku duniani vivyo hivyo ,uhalisia katika Vitendo ukiongezeka ndivyo hivyo tutaendana na mabadiliko ya yasayansi na technologia , hiyo ni kwa sababu mazingira ya sa sa yanataka mabadiliko .

Picha chanzo (professor Aaron Jackson)

1719053289138.png


Hivyo basi kwa kuhitimisha, niiombe serikali, taasisi zisizo za kiserikali pamoja makundi ya elimu kulizingatia hili kwani naona kama kutakuwa suruhisho kwendana na mabadiliko yanayotokea sasa duniani , na pia huwenda ikapunguza masuala ya ajira kwani watu wengi wanapoajiriwa ndipo wanaanza kupewa mafunzo (training ) ya kazi flani ,ambayo angepewa Bado anasoma kwa Vitendo huwenda angejiajiri na kutokana na unuji na maarifa aliyo nayo .
 
Upvote 2
Back
Top Bottom