Nafikiri hii imekaa kibiashara sana, kwani wanataka utumie Computer zao ili ulipie kuliko kuiba na kutolipia, Jiulize kama wewe ndo mwenye cafe unawateja wawili wanakuja watu kumi wana laptops zao wanataka kutumia bure utafikiliaje? Je utawakubalia watumie na wakati wewe toka asubuhi una wateja wawili tu?[/QUOT
Mkuu mie sioni tatizo hapo maana internet ni service na sio PC so kama mteja anakuja na notebook computer yake mie naona inamsaidia sana mwenye cybercafe maana PC zake zitakua hazitumiki... mteja ataconect kwa PC yake then alipe kama kawaida kulingana na muda anaotumia tena kama ndo mimi mwenye cybercafe ningetoa discount ya 10% kwa mteja anayekuja na notebook computer yake.....
Hapa TZ. Internate cafe nyingi haziruhusu kutumia. Laptops kwenye cafes zao na kama wanarusu basi bei ya muda wa kutumia huwa mara mbili zaidi kulinganisha kama ungetumia PC za cafe sijui tatizo liko wapi,naamini kutokana na mabadiliko ya nyakati ni muhimu watoa huduma au wamiliki wabadilike sioni kwanini kutumia Laptops mtu alipie mara mbili zaidi.
Hapo kijitonyama nafikiri ni Stambuli Internate cafe ipo jengo la Millenium karibu na mgahawa wa Steers,tatizo siku hizi hapo imekuwa kijiwe cha masuperstar wa bongo flavour wakija ni hadithi tu za nanihii ananibania,sijui produzya fulani kaiba wimbo fulani etc,pia siku hizi Stambuli Cafe si kama zamani net hukatika mara kwa mara na iko slow saana.Ila bigup kwa staff wa hapo cafe kwani wanajali wateja na huduma zao ni za weredi...Pale Kijitonyama kuna Cafe inafanya hivyo. Unaenda na Laptop yako wanakuchomekea kwenye outlet yao ya internet ila sina hakika kama wanakuchaji kwa muda ama per MB lakini naona wanapata wateja si haba.