regishirima
Member
- Oct 21, 2019
- 5
- 2
Moja kwamoja nianze kuelezea ninachotaka kuzungumzia, kama kichwa cha habari kinavyosema Upotevu wa Maji.
Huu upotevu wa maji ninao uzungumzia ni ule unaotokana na kuvuja kwa mabomba ya maji yanayo sambaza maji maeneo mbalimbali ya daresalam chini ya shirika la maji DAWASCO.
Kinacho nishangaza ni kwamba kila kona ambayo DAWASCO wamefikisha mtandao wao wa maji kuna mabomba yanavujisha maji. Yaani hakuna mtaa ambao utapita ukose bomba lina vuja maji iwe ni bomba kumbwa au ni dogo tena kuna maeneo mengine kuna mabomba makubwa yamepasuka na yanatiririsha maji mienzi zaidi ya mitatu bila hao wenye mamlaka ya maji kugundua.
Nayaandika haya kwasababu mimi ni fundi wa ujenzi na ninatembea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na kuyashuhudia haya.
Moja kati ya vitu vinavyoshangaza ni hao wasoma mita wanapita kila mtaa kwaajili ya kusoma mita na mabomba yaliyo pasuka wanayaona inamaana wanashindwa vipi kwenda kutoa taarifa ofisini kwamba mtaa fulani kuna bomba limepasuka.
Pia kuna hao mafundi wanao waunganishia wateja wapya maji nao wanayapita bila kufanya chochote ina shangaza sana. Haya yote yanasababishwa na uongozi kutokuwajibika vizuri nje ya ofisi wao wamekua wanakaa ofisini tu bila kutembelea mitaani wajionee hali halisi.
Pata picha bomba kubwa linavujisha maji zaidi ya mienzi mitatu tufanye yawe mabomba kumi yana vuja maji ikifika kiangazi huko yanakotoka yataacha kukauka kweli.
Maji yanapopungua huko yanakotoka walishajiuliza sababu ninini? Au wanakimbilia tu kutangazanga mgao
Mimi ninaami kwa upotevu huu mkubwa wamaji ninaoushuhudia kila ninapopita inaweza ikawa ni moja Kati ya sababu zinazofanya maji kupungua huko wanako yatolea.
Maja kati ya sababu zinazo sababisha uvujaji huu wa maji ni uunganishaji na uchimbiaji mbaya wa mabomba ya maji.
Mabomba mengi yamechimbiwa juu juu kiasi kwamba mtu akichimba jembe moha tu anaweza kulikata mengine yapo juu kabisa hata hayaja fukiwa kitu smbacho mda wowote linaweza kupasuka au kutobolewa.
Ushauri na maoni yangu kwa hao viongozi;
Ninawashauri waanzishe kikosi kazi maalumu cha mafundi ambao kazi yao itakua ni kufutilia na kurepea mabomba yalio pasuka tu ikiwezekana wawe na namba zao kabisa waziweke wazi ili mtu akiona bomba linalo vujisha maji awapigie wao moja kwa moja.
Hao wasoma mita na mafundi wanaounganishia watu maji wapewe maelekezo popote watakapopita wakiona bomba linalo vujisha maji waripoti kwenye hicho kikosi kazi ili iwe rahisi kufika eneo lenye tatizo.
Kingine uunganishaji na ufukiaji wa mabomba uwe ni wa kiwango kikubwa mitaro ya kufukia mabomba iwe na kina kirefu ili kuepuka ajali za kupasuka mabomba mara kwa mara.
Mwisho.
0625409082

Upvote
0