Kiuhalisia sisi wananchi wa kawaida ni kama shamba la bibi jamaa wanatusulubu kwa kulipa KODI, ADA, TOZO, FAINI, MAKATO n.k
Hebu fikiria mtu kabla ya mshahara kukufikia kwa kiganja hii mijamaa inautumbulia mimacho na kuvuna asilimia zao kama kazi walifanya wao vile..,
Unakuta wamekata PSSSF 5% au NSSF 10%, PAYEE 12%, HESLB 15%, NHIF 3%.
Mshahara ukikufikia sasa kuna indirect taxes kwa kila bidhaa utake usitake utalipia, kuna kodi ya nyumba/chumba cha biashara, kuna ada na tozo kwa kila pesa utakayofanya muamala/miamala hapo ukumbuke hata ule mshahara wako walioulima PAYEE still ukitaka kutoa pesa bank lazma watakukata ada na tozo za kuitoa huko bank.
Sasa kama unakamkebe kako used from Japan unadrive kuepuka adha ya public transport ndio utajuta zaidi maana utakutana na faini zaki hopeless plus hizo parking charge kama vile silipiagi kodi kwenye nchi yangu.
Oyaa hii parking charge ni wizi kama wizi mwingine tu.