SoC02 Kutozingatia utaalamu, chanzo ukosefu wa ajira kwa wasomi Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Dibwi Method

Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
31
Reaction score
28

Na Dibwi

Tafiti mbalimbali duniani, zimeonyesha Bara la Afrika na Asia kuongoza kwa kuwa na utitiri wa Mashirika na Taasisi nyingi hasa zile za Umma, kutozingatia suala la kuajiri watendaji walio na elimu, utaalamu na uzoefu mahususi kwenye nafasi husika kwenye maeneo ya kazi.

Hali hii inatokana na waajiri wengi kujikita zaidi kwenye kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara zao kuliko kuzingatia ubora wa juu na ufanisi kutoka kwa watendaji wao.

Matokeo yake, yeyote anaweza kufanya kazi yoyote ile bila kujali ujuzi, uwezo, elimu wala uzoefu unaohitajika kwenye kazi husika.

Nchini Tanzania, hali hii imekithiri sana na imeathiri soko zima la ajira hasa kwa wataalamu na wasomi ambao wameenda vyuoni kwa miaka kadhaa ili kusomea fani husika kwa malengo ya kuajiriwa hapo baadaye. Kila mwaka, vijana zaidi ya laki mbili huhitimu kutoka vyuo vikuu mbalimbali na vile vya kati kwa ngazi ya astashahada na shahada, kwenye kada mbalimbali kama vile: Uhasibu, Ualimu, Utabibu, Utawala, n.k.

HALI SIO SHWARI!
Limekuwa ni jambo la kawaida sana kumkuta mtu mwenye elimu ya fani ya ualimu akiwa ameajiriwa kama Mhasibu benki au mtaalamu wa afya kufanya kazi za uandishi wa habari.

NINI CHANZO?

Mambo makubwa manne yamekuwa mstari wa mbele katika kkuchochea hali hii nchini Tanzania, kwani kila kukicha ni afadhali ya jana!

Moja, unayemjua, kwa kiingereza inajulikana kama ‘technical know who’, ni bora kuliko ulichonacho kichwani, au ‘technical know-how’ Siku za karibuni imeibuka changamoto hii, kama huna ‘konecshen’ mtu unayemjua basi fani yako itabaki kwenye makaratasi. Utaalamu umekuwa hauzingatiwi sana maeneo ya kazi na badala yake kama unafahamiana na mwajiri, hiyo ndo inakuwa tiketi ya kupata ajira. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hali hii imeshamiri sana kwenye mashirika mengi ikiwa ni pamoja na taasisi nyingi za Umma. Mungu amsaidie sana mtoto wa mkulima ambaye hana anayemfahamu zaidi ya jembe la kulimia shamba la ukoo wake!

Pili, unafuu wa gharama, kutokana na kodi nyingi, tozo na makato makubwa yanayotozwa kwa makampuni nchini ili kutengeneza faida, waajiri wengi kwenye sekta binafsi nchini, hulazimika kujikita zaidi kwenye kupunguza gharama za uendeshaji kiasi kwamba wako tayari kuajiri watu wenye uwezo duni ambao wako tayari kulipwa ujira mdogo kuliko kawaida.

Tatu, mfumo mbaya wa elimu, kila mwaka, vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini huzalisha wataalamu zaidi ya laki mbili. Mitaala yetu ya elimu imetengenezwa kuwajengea vijana uwezo wa kukariri na sio kuwa wabunifu. Hali hii imepelekea vijana wengi baada ya masomo, kuwa tayari kufanya kazi yoyote ili tu kujiingizia kipato. Matokeo yake maadili ya fani mbalimbali yamekuwa hayazingatiwi kwenye maeneo ya kazi kwa kukosa watu sahihi.

Nne, sera mbaya za nchi, mpaka sasa sera nyingi za ajira nchini hazina meno, zipo kwenye makaratasi tu bila vitendo. Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 1996, inasema, ‘Vijana wake kwa waume, ndio wenye nafasi nzuri na uwezo mkubwa wa kuendelezwa na kupatiwa maarifa na ujuzi ikiwa ni pamija na kushirikishwa katika utoaji wa maamuzi mbalimbali. Utaratibu wa kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi ni ule wa kuwashirikisha watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi katika kupanga, kuamua na kutekeleza shughuli ambazo zitawawezesha kuinua hali zao za maisha’. Ni ukweli usiopingwa kuwa Sera hii haitumiki kabisa kwani kiwango cha ushirikishwaji wa vijana kama invyoeleza ni kidogo sana kama hakipo hakiba. Hii sera ukiisoma, inakupa matumaini sana, lakini haina utendaji wowote ule kwani Wanasiasa ndio wamepewa dhamana ya kumfanyia kila Mtanzania maamuzi kwenye kila sekta.

Maoni ya wanasiasa wengi hasa Wabunge wamekuwa wakitoa maoni ambayo yanakatisha tamaa. mara kadhaa wamenukuliwa wakisema “Vijana wasingoje tu kuajiriwa bali wajiajiri” Maneno kama hayo ni kejeli kubwa sana na yanapaswa kukemewa! wanashindwa kutilia maanani mikopo mingi inayotolewa kwa masharti magumu na riba kubwa sana, miundombinu mibovu kwa wajasiriamali wadogwadogo hasa machinga ushuru usiozingatia kipato, sheria na kodi za hovyo zinazoondoa mazingira wezeshi ya kujiajiri.

ATHARI ZAKE
Kwanza
, wataalamu na wasomi wengi (hasa vijana) wenye uwezo wamejikuta bila ajira huku watu wachache wasio na uwezo wakineemeka. Wiki chache zilizopita, tumeshuhudia aliyekuwa Inspecta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro ambaye kwanza tayari amefikia umri wa kustaafu, akipewa Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Pili, misingi ya kazi ya Ubalozi haijazigatiwa kwani kwa misingi ya Uaskari ni maji na mafuta. Tatu, je, ni nini hatma ya vijana wengi sana ambao wamesomea na wanaosomea diplomasia na wale ambao tayari wana uzoefu wa kazi (Career Diplomats)? Hii inawapa picha gani?

Pili, kukosekana kwa ufanisi na ubunifu Serikalini na kwenye mashirika ya Umma. Ni zaidi ya miaka sitini sasa tangu nhci hii ijipatie Uhuru wake kutoka kwa Wakoloni. Inasikitisha kuona mpaka sasa bado tunahangaika na mambo kama umeme, maji safi na salama na magonjwa kama maralia. Nchi kama Korea Kusini ambazo kiuchumi tulikuwa sambamba kwenye miaka ya sabini, kwa sasa wako mbali sana kwenye nyanja za teknolojia, sayansi na kilimo kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya kwenye tafiti nyingi na za kimaendeleo.

Tatu, matabaka, walio nacho wanazidi kupata zaidi na wasionacho wanazidi kupokonywa hata kile kidogo walichokuwa nacho. Kiongozi mmoja mkubwa nchini aliwahi kunukuliwa akisema kwamba wanachaguliwa watu wa familia ambazo tayari zipo kwenye mfumo kwa sababu wana asili ya kutawala kama ilivyokuwa kwa wazazi wao. Kwa tafsiri, ya haraka na nyepesi ni kwamba kama kijana hana ndugu au wazazi ambao wamewahi kuwa kwenye mfumo, itakuwa ngumu sana kwake kushika nafasi za juu serikalini, haijalishi uwezo, utaalamu, uzoefu na elimu aliyonayo. Kwa akili za namna hii, sihitaji kupiga ramli ili kujua ni kwanini hata baada ya miaka zaidi ya sitini toka tumepata Uhuru bado tumekwama. Inasikitisha sana!

Nne, kukosekana kwa maadili kwenye maeneo ya kazi na kupelekea vitendo vya rushwa kukithiri. Uhalifu umekuwa ukiongezeka kila kukicha nchini. Kama ilivyo ada, serikali kupitia Jeshi la Polisi wametangaza vita kwa makundi ya kihalifu kama Panya Road na mengineyo. Kutangaza vita sio mwarobaini wa kutibu uhalifu nchini, kuna haja ya kuangalia namna sahihi ya kukata mizizi inayopelekea uhalifu ambayo ni umasikini na ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, ambayo kwa pamoja yanaopelekea umasikini. Hakuna mtu ambaye anazaliwa akiwa na asili ya uhalifu bali ni ugumu wa maisha ndo unapelekea mambo kama wizi, ujambazi, utapeli n.k. “Vijana walio wengi, asilimia 60 ya wale wote wasio na ajira rasmi nchini hawana kazi maalum. Matokeo yake baadhi yao hujiingiza katika vitendo kama vile wizi, ujambazi, uvutaji bangi, uzururaji, utumiaji madawa ya kulevya, umalaya n.k. Aidha vijanawameendelea kuwa tegemezi kwa wazazi wao hasa katika maeneo ya mijini’ (Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, 1996)

Karibu Mwanajukwa , tujadiliane kwa pamoja juu ya namna ya kutatua changamoto hii kwa mustakabali wa nchi yetu!

Upvote 13

Nime kupigia kura
Ninashukuru sana kaka
 
Kwa uandishi wa kina hivi, kwanini usipewe column kuandikia magazeti kabisa🔥..utufikishie kilio chetu Kwa wahusika
 
Kwa uandishi wa kina hivi, kwanini usipewe column kuandikia magazeti kabisa🔥..utufikishie

Jambo hili limekua changamoto, mashairi standards za uajiri zifuatwe na watu wenye position wawe na hofu ya Mungu na kufanya majukumu kama wanavyotakiwa na siyo kama wanavyotaka wao. Haki ikifiatwa itasaidia kupunguza changamoto hii na badae kuimaliza kabisa.
 
Back
Top Bottom