Hivi na nyie wengine mnao ndugu wasio na shukrani?
Ndugu ambao hukukumbuka wakati wa shida zao tu?
Huwa mnakabiliana nao vipi watu wa aina hiyo?
Mimi wananikera sana kwa kweli.
Mtu anakuja na kukulilia shida zake lukuki, nawe kwa moyo mweupe kabisa unamsaidia.
Tena unamsaidia kwa kwenda mbali zaidi ya kile alichokiomba.
Cha ajabu [ingawa si ajabu kivile] ukishamsaidia tu, mwenzio anapotea.
Anapotea bila hata kutoa 'ahsante' ya msaada uliomsaidia.
Na akishapotea ndo imetoka hiyo. Kuja kusikia tena toka kwake labda ni awe na shida au kwenye msiba.
Hata salamu tu ya kujuliana hali toka kwake inakuwa tunu.
Naamini katika kutenda wema na kwenda zangu lakini pia sipendi mambo ya kufanyanya wapumb.avu.
Yaani kuniona nakufaa tu wakati wa shida zako. Ukiwa huna shida hata simu zangu hupokei.
Hovyo kabisa hao.....