Kwahiyo mafanikio ya serikali si yanaelezewa kwa hoja? Ama unadhani alichokisema katibu mkuu hakitokei? Unataka kusema ccm inatumia serikali dhidi ya upinzani na polisi wanawatumiaje?Mimi ninachojua ,Bashiru alikuwa anaiongelea dola(serikali) na sio vyombo vya dola (polisi n.k). Mafanikio ya serikali ndio uhakika Wa chama chenye madaraka kuendelea kutawala kwa kuwa serikali ndio dola inayochaguliwa na watu.
Well said mkuu!Midahalo inapima uwezo wa kujieleza kwa kiongozi anayekusudia kuomba nafasi kubwa za uongozi,na lengo ni kujua na kutambua uwezo wa huyo kiongozi tarajiwa kwenye mambo mbalimbali ya kidunia ili ikitokea amepewa nafasi ya kuongea kwenye mikutano ya kimataifa asibabaike au kuogopa mikutano ya kimataifa. Ni aibu kwa nchi kuwa na kiongozi parochial kwenye mambo ya kidunia maana Rais ni nembo ya Taifa akiwa empty minded ni sawa na kuwa nchi na wananchi wake ni empty minded pia
Bila Dola ni wepesi kweli kweli. Ccm ni chama dola. Kinaiongoza nchi yetu kifashisti. Ukiona chama kinaweza kuleta watu wanaoonekana kama vichaa ujuwe kuna tatizo pahala.Kwa hiyo ili msalie Madarakani mnategemea dola..?
Mkuu ccm ni dola na dola ni ccm! It is reciprocal! Ndo maana unaona wanajeshi na mapolisi, sambamba na viongozi wengine kwenye majeshi yetu, kufadhiliwa na kupewa vyeo na serikali ya ccm mara baada ya kustaafu. Wengine wanaingizwa kwenye nafasi za kiutendaji serikalini, mfano ukuu wa mkoa nk.Unataka kusema ccm siyo chama cha siasa bali ndiyo dola yenyewe siyo ?
Hivi ccm bado kinaweza kusimamia hoja ipi kwa sasa na kikawashawishi wananchi ?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki chama hakifai tena. Ni vyema kikafa tuanze upya. Au kuwepo na katiba mpya. Chini ya mfumo huu tutakuja kujuta sana huko mbeleni. Kama tukiponea kuingia kwenye full dictatorship tushukuru sana. Lakini huu ndo wakati ambao mapungufu karibia yote ya mfumo huu yanaonekana na kufahamika na walio wengi.CCM imechokwa hata kijenge barabara zilizinakshiwa kwa Dhahabu bado Wananchi wanataka mabadiliko
CCM hawawezi kushindana na wakati nyakati zimebadilika sana sana
Chama hiki cha kukomunisti hata kikija na mbinu gani bado kitang'oka tu
View attachment 1379053
Hapa kwa kifupi umesema kwamba ccm haiwezi kuacha kutumia dola dhidi ya wapinzani wa kisiasa.Kwa ujumla katibu mkuu wa ccm amekuwa mkweli. Vyama mbadala vitumie uelewa huo kupanga mikakati mbadala. Kwa mfano kutafisiri sheria na kuzikomalia kwa nguvu ya umma. Wasisahau kutakuwa na gharama hadi ya maisha ya watu.
Ebu weka hiyo kauli hapa tuione. Kwani wewe umeelewa vipi? Sina nia ya upotoshaji.Mimi nadhani hamkuelewa kauli ya katibu na tatizo letu watanzania kila kauli kutoka ccm uwa tunaichukulia kipinzani naomba ukasikilize tena maana Juma kaparatu aliomba katibu aweke sawa maelezo na aliongea vizur usipotoshe uma
Sent using Jamii Forums mobile app
Asilimia zaidi ya tisini ya wananchi wa Tanzania ni wakulima. Badala ya kuwaeleza wakulima utawasaidia vipi, wewe unachagua kutumia dola na wala huna haja ya kutumia hoja kwasababu wananchi hawajitambui? Wanachokifanya ccm kinaonyedha dharau kubwa sana kwa wananchi na ni sawa na kuutukana ufahamu wetu!Hiki Chama kinajieleza kuwa kinawatetea wakulima na wafanyakazi ukiangalia vizuri wakulima wanamaisha duni ya kutisha na wanazidi kuwa masikini hali kadhalika wafanyakazi mishahara haiongezwi mifuko yao ya pensheni inakombwa na kuporwa fedha na CCM
CCM kinatetea matumbo yao na kwa mujibu wa Katibu wake mpya anasema kuwa Chama hakitakabidhi madaraka kwa Watanzania hiyo ni kauli ya kushindwa.
Jinsi wanavyojitetea, ndivyo wanavyozidi kujifunga! Madai yao yangekuwa na ukweli wowote, basi tusingeona hila na unyanyasaji dhidi ya wapinzani.Halafu wengine wanamtetea eti tumemuelewa vibaya...msomi kama yeye anawezaje kusema vitu halafu hadhira isielewe..??
Hoja yake ni mfu, eti anadai kuwa ccm kutumia dola na taasisi nyingine za umma ndiko kumeleta amani nchini. Hao ni wale waliokunywa maji ya bendera ya chama cha kifashisti.Huna lolote upeasant tu umekujaa, unafananisha vitu visivyo fanana.
Policeccm ndio wanawabeba,ndio mana police n traffic awamu hii wanachukua rushwa hadharani mana wanajua meko anawategemea wao kutawala
Sent using Jamii Forums mobile app
Chama kilichowekwa madarakani kwa ahadi ya kuwakomboa watanzania sasa kimekuwa Chama cha wababe kinatawala kimabavu na kufikia kuuwa watanzania wanaokikosoa hata wenye kuhoji Phd ya kiongozi wanaishia kwenye Chainsaw CCM kimekosa uhalali wa kuiongoza nchi hii sasa kinatumia Polisi na vyombo vingine katika kuliteketeza taifaAsilimia zaidi ya tisini ya wananchi wa Tanzania ni wakulima. Badala ya kuwaeleza wakulima utawasaidia vipi, wewe unachagua kutumia dola na wala huna haja ya kutumia hoja kwasababu wananchi hawajitambui? Wanachokifanya ccm kinaonyedha dharau kubwa sana kwa wananchi na ni sawa na kuutukana ufahamu wetu!
ccm ingewasaidia wakulima kidogo tu bila kujali matumbo yao nchi ungekuta iko mbali sana! Kwanza hivyo viwanda ungekuta vina uhitaji bila kulazimishiwa. Wao wamebakia na bombadia na hawataki kuhojiwa na huku wanachokifanya ni kuzitolea maamuzi pesa zetu wananchi bila ya kutushirikisha. Mfano kungekuwepo na midahalo ingesaidia sana! Na mfumo huu utakufa ccm ikifa.