Kutumia Till ya M-Pesa & Tigo Pesa zenye majina ya watu wengine

alsaidy

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Posts
334
Reaction score
89
Wakuu,

Nina mpango wa kuanzisha biashara ya M-Pesa na Tigo Pesa. Kutokana na ugumu wa kupata hizo till inakulazimu kutumia till zenye majina ya watu wengine.

Naomba kujua kama kuna risk yoyote inayoweza kutokea kwa baadae na je ukiwa na tatizo inakuwaje unapokwenda kuripoti?

Naomba wenye ujuzi na waliopitia mambo haya wanijuze kuhusu hili.

Natanguliza Shukrani.....
 
Till ni sim card ambayo imekuwa programed ku support tigo pesa au m pesa. In other words are special sim card which supports pesa sevice..
 
Till ni sim card ambayo
imekuwa programed ku support tigo pesa au m pesa. In other words are
special sim card which supports pesa sevice..

ofcouse swali zuri nami nasubiri kujua kupitia majibu ya waungwana
 
tatizo litakuja pale,till itakapo potea,na kutakiwa kwenda kui renew hutaweza mpaka umtumie muhusika mwenyewe kwenda kufanya kazi hiyo!je kama aliyekuachia hiyo till amefariki itakuwaje?kingine kama till yako ile ambayo unawekewa commision pesa zimekuwa nyingi hutakuwa na uwezo wa kwenda bank(ambayo ni wakala wa kampuni hiyo ya simu)kutoa hizo pesa,yaani umrushie salio akupe cash,kwani utatakiwa kitambulisho husika!Cha kufanya we mwambie mwende naye akabidilishe jina,ili u2mie la kwako,japo si kiofisi direct ni kwaku2mia magumashi(uwape hela ya maji)wanabadilisha tu.We jaribu kufanya risk analysis,uamue kipi ni bora.
 
Btw,
What is "Till"??

Till(au vibati)ni mfano wa line za simu,ambazo kwenye biashara ya m-pesa,tigo pesa,airtel money na ezy pesa,zina kuwa mbili,ambazo wakala unapewa na kampuni husika.moja inakuwa ya kazi ambayo ndiyo itatumika kutolea huduma kwa wateja ktk kuweka na kutoa,inakaa eneo la biashara,(ambayo ndio namba yako ya uwakala)till ya pili,ni ile ambayo unapokwenda kununua salio lako we wakala iwe bank au kwa wakala wako mkuu ndipo hilo salio litaingizwa, kisha we ndio ulihamishie kwenye till yako ya kazi(namba yako ya uwakala),na commision zako zote zinaingizwa humo,na unakuwa na uwezo wa kui control till namba moja,kama kuangalia salio lililopo, hata kama upo mbali na eneo lako la biashara,kwani hiyo c ya kumuachia mfanyakazi,unakuwa nayo wewe,na hata kama mfanyakaz analeta ujanja unjanja unauwezo wa kuihamisha pesa yote iliyomo kwenye till ya kazi na kuileta kwenye till namba 2.
 
risk inakuja kunapokuwa na umuhimu wa utambulisho kama wadau walivyokujuza hapo juu ,,,kwa kifupi unakuwa illegal owner wa hiyo till numbe na kukosa uhalali wa kisheria kunapotokea chochote kama vile upotevu wa fedha n.k
 
Mkuu nashkuru sana kwa maelezo yako mazuri na muhimu. Ni kweli Till ya m-pesa nimeipata baada ya kutoa kitu kidogo na wanakupa line mbili kama maelezo yako ulivyoyaweka. Kwa tigo-pesa kwa maelezo ambayo nimeyapata mpaka sasa ni kuwa wao wana line 1 tu na sio mbili kama m-pesa.

Naomba kujuzwa ukweli ni upi?
 
risk inakuja kunapokuwa na umuhimu wa utambulisho kama wadau walivyokujuza hapo juu ,,,kwa kifupi unakuwa illegal owner wa hiyo till numbe na kukosa uhalali wa kisheria kunapotokea chochote kama vile upotevu wa fedha n.k

Ni kweli unachozungumza mkuu, ila hao jamaa ambao ndio wanataka kunipa hizo line wameniambia hakuna tatizo kama itatokea lolote lile niwaarifu then wao wanajua wata solve vipi.

Ila kwa tigo-pesa jamaa yuko tayari kubadilisha jina na mnaandikiana mkataba na inachukua muda wa mwezi na ushee. Kwa mujibu wa jamaa wa tigo-pesa wanachotaka kuona kama kuna mabadiliko ya umiliki basi hiyo till ifanye biashara zaidi kinyume na hapo wanakuwa wakali.
 
unamaanisha hiyo kitu inafanyika official kabisa kwenye ofisi zao au ndiyo janja ya mjini mjini?
 
Ni official mkuu kwa sababu nilivyomuelewa mimi huyu jamaa ndio ilikuwa kazi yake ya kutoa uwakala wa tigo-pesa na ni muajiriwa wa tigo. Kinachofanyika anakwenda kwa super agent na kumpelekea maelezo pamoja na vielelezo vyangu (TIN,Leseni ya biashara vitahitajika kubadili jina)na hapo super agent ata badilisha jina ila tu iwe till hiyo inayobadilshwa jina ina fanyakazi vizuri kuliko hapo awali ilivyokuwa.
 
hapo kama hujaambiwa utoe laki ,basi ni laki na nusu au laki 3
 
Mkuu ni pesa ndefu kidogo kwani hakuna njia nyingine ya kupata hiyo till ya tigo pesa. Ukizingatia kwa sasa hazitoki kabisa ni kununua till kwa mtu apart from that there is no other option...
 
ya official haina gharama ,hiyo ni ujanja wa mjini tu......... kuwa mvumilivu ufuate utaratibu wa kawaida au kubali kuliwa hela ambayo hujui utairudisha vipi........
 
kama unahitaj till ya m pesa andaa laki 5 bila float,nitafute kwa 0716030083
 
Back
Top Bottom