Till ni sim card ambayo
imekuwa programed ku support tigo pesa au m pesa. In other words are
special sim card which supports pesa sevice..
Btw,
What is "Till"??
Till(au vibati)ni mfano wa line za simu,ambazo kwenye biashara ya m-pesa,tigo pesa,airtel money na ezy pesa,zina kuwa mbili,ambazo wakala unapewa na kampuni husika.moja inakuwa ya kazi ambayo ndiyo itatumika kutolea huduma kwa wateja ktk kuweka na kutoa,inakaa eneo la biashara,(ambayo ndio namba yako ya uwakala)till ya pili,ni ile ambayo unapokwenda kununua salio lako we wakala iwe bank au kwa wakala wako mkuu ndipo hilo salio litaingizwa, kisha we ndio ulihamishie kwenye till yako ya kazi(namba yako ya uwakala),na commision zako zote zinaingizwa humo,na unakuwa na uwezo wa kui control till namba moja,kama kuangalia salio lililopo, hata kama upo mbali na eneo lako la biashara,kwani hiyo c ya kumuachia mfanyakazi,unakuwa nayo wewe,na hata kama mfanyakaz analeta ujanja unjanja unauwezo wa kuihamisha pesa yote iliyomo kwenye till ya kazi na kuileta kwenye till namba 2.
risk inakuja kunapokuwa na umuhimu wa utambulisho kama wadau walivyokujuza hapo juu ,,,kwa kifupi unakuwa illegal owner wa hiyo till numbe na kukosa uhalali wa kisheria kunapotokea chochote kama vile upotevu wa fedha n.k
Ni kweli unachozungumza mkuu, ila hao jamaa ambao ndio wanataka kunipa hizo line wameniambia hakuna tatizo kama itatokea lolote lile niwaarifu then wao wanajua wata solve vipi.
Ila kwa tigo-pesa jamaa yuko tayari kubadilisha jina na mnaandikiana mkataba na inachukua muda wa mwezi na ushee. Kwa mujibu wa jamaa wa tigo-pesa wanachotaka kuona kama kuna mabadiliko ya umiliki basi hiyo till ifanye biashara zaidi kinyume na hapo wanakuwa wakali.
unamaanisha hiyo kitu inafanyika official kabisa kwenye ofisi zao au ndiyo janja ya mjini mjini?
Ni official mkuu kwa sababu nilivyomuelewa mimi huyu jamaa ndio ilikuwa kazi yake ya kutoa uwakala wa tigo-pesa na ni muajiriwa wa tigo. Kinachofanyika anakwenda kwa super agent na kumpelekea maelezo pamoja na vielelezo vyangu (TIN,Leseni ya biashara vitahitajika kubadili jina)na hapo super agent ata badilisha jina ila tu iwe till hiyo inayobadilshwa jina ina fanyakazi vizuri kuliko hapo awali ilivyokuwa.
hapo kama hujaambiwa utoe laki ,basi ni laki na nusu au laki 3
Mkuu ni pesa ndefu kidogo kwani hakuna njia nyingine ya kupata hiyo till ya tigo pesa. Ukizingatia kwa sasa hazitoki kabisa ni kununua till kwa mtu apart from that there is no other option...