Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Bandugu,
Zulia jekundu ni zulia ambalo limezoeleka kutumika katika shughuli maalumu. Kwa shughuli za serikali, hili hutumika kwenye hafla za kitaifa na kunapokuwa na ugeni kutoka nje.
Katika Uchaguzi Mkuu huu, kuna mgombea mmoja wa Urais ambaye katika majukwaa yake kunatandazwa zulia jekundu.
Kwa mtazamo wangu hii ni uthibitisho wa kutotambua maana ya tukio husika au dalili za mtu aliye out of touch na maisha ya wtu wa kawaida.
Hili la kuzunguka mikoani na mazulia halafu unayatandaza kwenye vumbi, bado sijaelewa kwa kweli hata katika safari za Rais za mikoani.
Wanasiasa wetu watabadilika lini? Lakini zaidi wananchi wataamka lini ili wapewe heshima wanayostahili? Hapo sijaongelea kuwasimamisha wananchi kwenye jua wakati waheshimiwa wamekaa kwenye viti vya enzi kivulini?