Donathageorge88
New Member
- Jul 16, 2021
- 1
- 0
Ni jioni tulivu kabisa, naamua kuperuzi mtandaoni kupitia simu yangu ya kiganjani. nakutana na tangazo kutoka jamii forums linalohusu stories for change, ambalo kama nitaamua kushiriki napaswa kuandika kuhusu Tanzania ninayoitaka miaka kuanzia mitano ijayo.
Najihoji je! nataka Tanzania ya namna gani miaka ijayo nini kisaidie katika uchumi,elimu,afya na megineyo? Naumiza sana kichwa nikitafakari niandike nini au juu ya jambo gani, Kisha nikakumbuka mwaka 2023 nilitamani kuandika kuhusu Tabia na Nidhamu vinavyoweza kuleta mabadiliko makubwa katika maeneo mbalimbali yanayohusu nchi yetu kwa ujumla.
Watanzania ni watu tuliozoea kufanya mambo kwa mazoea sana. niliwahi kwenda mahala fulani kwa muda ambao nilikua nimeelekezwa kufika kwasababu ofisi hizo nilijulishwa kuwa zinafunguliwa kuanzia saa moja na nusu asbui. Hivyo basi nilijihimu sana kabla ya saa moja na nusu nilikua nimekwisha kufika. nilifika na kuona kuwa ofisi ile zilikua bado hazijafunguliwa, nilijaribu kuhoji kwa watu waliokua wakipita maeneo hayo, nikajulishwa kuwa ofisi hizo hufunguliwa kwa kuchelewa sana na muda mwingine hufunguliwa saa nne asbui. Jambo hili lilinihuzunisha sana kwamba imekua ni jambo la kawaida kwa watanzania kuchelewa kufungua hata ofisi za umma.
Wakati mwingine niliwahi kwenda duka fulani kwaajili ya kununua mahitaji madogo madogo ya nyumbani, nilipofika dukani nilimkuta binti ambae alikua ameshikilia simu na hata niliposalimia aliendelea kutumia simu yake akinihoji nahitaji nini? nikamwambia nahitaji sukari na mafuta ya kula. aliinuka akawaambia watu alokua nao kwa simu nipeni dakika moja nimtoe mtu hapa kabla mb zangu hazijaisha. Aliniwekea vitu kwenye mfuko mdogo kisha akataja gharama yake akiwa amekasirika sana na kunitaka nilipie kwa haraka. Nilimuuliza kama anauza unga kwa kilo akanijibu ndio nikahoji ni kiasi gani gharama ya unga akasema bei iliyo kubwa kuliko bei elekezi, nilipomhoji kwanini bei yake ni tofauti nabei elekezi?, alinambia, nenda duka lingine kama hauna hela unauliza ili iweje?
Akaendelea kuongea na simu akiwa mubashara kwenye moja ya mitandao ya kijamii nikiwa naondoka nilimsikia akiwaambia wenzie, wateja wengine wasumbufu sana kunikatia tu mood yangu,kama mtu huna hela unaenda dukani kufanyaje? nilisikia kauli ile vyema kabisa na nikajiapiza sitorudi dukani pale wakati mwengine.
Wakati mwingine nilikua nimekaa mahala wanapouza kahawa, ni mgahawa maarufu mjini posta dares salaam. mara nikaona mzungu akiangalia saaa yake mara kwa mara. alionekana mwenye haraka na alikua akimsubiri mtu fulani waweze kuonana. lakini ilionyesha kuwa yule aliekuwa akisubiriwa amechelewa sana hivyo kumfanya mzungu yule kuwa na hasira kidogo. baada ya dakika kumi na tano mzungu yule aliondoka. baada ya nusu saa kuna mwanaume alikuja akawa anawahoji wahudumu je mmemuona mtu mzungu alikuwepo hapa? wakamjibu ndio amekwisha kuondoka. mwanaume yule alijilaumu sana kwa kuchelewa kwake na alikata tamaa ya kuonana na mzungu yule.
Kuna wakati niliwahi kusoma na kusikia kutoka kwenye vyombo vya habari kuhusu vijana walokua wamegundua umeme na wengine niliwaona kwenye maonyesho ya nane nane wakionyesha ujuzi wao wa kumwagilia shamba kwa kutumia simu. Baada ya muda sikuwasikia tena.
Mabadiliko yatakuja kama sisi watanzania tutaamua kubadilika katika haya maeneo makuu mawili yafuatayo;
1. Kumjali mteja ambae anakuja kwaajili ya kupata huduma au kununua bidhaa ni jambo ambalo ndilo muhimu na litaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali nchini kwetu. namna tunavyowahudumia na kuwauzia watu bidhaa na huduma mbalimbali itawafanya watu hawa kutoa sifa mbaya au nzuri kuhusu huduma na bidhaa tunazouza. kama mjuavyo sifa mbaya huvuma zaidi kuliko njema na wateja hununua kutokana na sifa alizosikia kuhusiana na huduma au bidhaa fulani. anapofanya maamuzi ya kuja kununua kisha akahudumiwa vibaya anawezea asirudi tena. mfano hospital namna inavyopokea watejana kuwahudumia ikiwa itatoa huduma mbaya au kuwahydumia wagonjwa ambao ndio wateja wao vibaya inaweza kukosa wateja wao kwa kipindi kirefu hivyo ikafungwa kwasababu haitopata mapato ya kujiendesha.
Huduma ya kuwajali wateja wa nje na wandani inapelekea wateja wengi kupendelea kutumia huduma au bidhaa yako hili litaongeza uchumi wa mtanzania mmoja mmoja au taifa kwa ujumla. Sentensi kama karibu nikusaidie nini siku ya leo? oh samahani hatuna huduma, hiyo hapa naomba nikuonyeshe mahali utaipata kwa urahisi. asante karibu tena wewe ni mteja wetu maalum. asante kwa manunuzi uliyoyafanya. hizi ni kauli ambazo zinamfanya mtu atoe sifa nzuri juu ya biashara fulani au huduma fulani.
Kuna hospital ya kiserikali ambayo sikuwahi kujua kuwa ni nzuri, kuna wakati nililalamika juu ya maumivu ya jino kwa mfanyakazi mwenzagu akanielekeza hospital hiyo. nilienda na kupokelewa vizuri sana na kutibiwa, sasa nimekua kama balozi wa kujitolea nikiwaabia watu namna hospital hiyo inatoa huduma nzuri za meno.
2. Kujali muda ni tatizo la watanzania wengi sana. na imeonekanna kama ni jambo la kawaida sana. unakuta mtu anasema hili tukio limeandikwa saa nane ila najua kuwa watu wataanza kuja saakumi so nisije kuwahi watu wakachelewa nikaaa mwenyewe kwa muda mrefu. kama watanzania tumekua tukikosa fursa nyingi kwasababu ya kutotunza muda.
Watu wengi hupoteza fursa na nafasi kwasababu hupuuzia hili eneo sana. Jambo la kusikitisha Zaidi ni pale linapochukuliwa kama suala la kawaida kabisa na mara nyingine hutoona mtu aliechelewa akijutia uamuzi wake au kuchelewa kwake. Kuna mahali niliambiwa nipeleke bidhaa flan nilipofika dakika kumi kabla ya ule muda nilioelekezwa walinambia wao wametoka sababu washajua kuwa watanzania huwa hawatunzi muda hivyo niwasubiri.
Watanzania wakianza kumaanisha katika kutunza muda mambo mengi yataenda kwa wakati na kutatuliwa kwa wakati sababu kila mtu atajali na kutunza muda wa wengine. Na ndani ya masaa 12 ya kazi kama huduma zitatolewa kwa wakati,zitatolewa kwa uzuri na zitatolewa vizuri katika sekta mbalimbali nchini nchi yetu itabadilika na tutaona matokeo chanya ya haraka yakiambatanishwa na maendeleo ya kiuchumi na teknolojia.
Na hiyo ndio Tanzania niitakayo mimi, Tanzania ambayo watu wanatoa huduma nzuri kwa wakati sahihi wakiwajali wanaowahudumia na kuwapa huduma kwa wakati unaotakiwa na kuwa wakweli katika kutunza muda. Hii itapelekea watanzania kupata mapato makubwa kwa wakati hivyo kuipa serikali kodi kwa wakati jambo litakalopelekea maendeleo ya haraka kuwepo katika jamii yetu.
3. Serikali inatakiwa baaada ya kutambua vijana wa aina Fulani wana vipaji flani ni vyema ihakikishe ule ujuzi wao haupotei, wawadhamini na kuhakikisha ugunduzi wao unatumika hapa Tanzania kwa faida ya watanzania. Wasiwakamate na kuwaonya au kuwatishia wanapokua wamegundua vifaa mbalimbali, bali kama ikiezekana kuwaajiri serikalini ili kuisaidia serikali katika shughuli zake. Hiyo ndio Tanzania niitakayo.

Upvote
1