Kuuliza Multiple Choice Question katika University Exams: Tunapima nini?

Ni vyuo vya Tanzania tu wanaendekeza huu upuuzi mimi nimesoma UDSM (Bachelor Degree), Univ. of Cape Town (Master Degree) na South Hampton (Master ya 2) na Short courses vyuo vya Netherlands na USA sijawahi kuona huu upuuzi wa MULTIPLE CHOICE. Nimefanya utafiti vyuo vya Kenya & Uganda hawana huo utaratibu. Nyie wa-TZ endeleeni kujifariji tu na uj.Inga wenu
 

Upo sahihi;
ishu ni kuwa majibu sahihi huwa ni zaidi ya moja na kulazimika kusugua kichwa kubaini jibu sahihi zaidi..Ukitoka kwenye paper kichwa kidogo lazima Umeze kidonge cha kutuliza Maumivu.
 
Leo mnasifia MCQs za vyuo vikuu wakat huo huo mnaponda utaratibu wa mitihan ya darasa la saba kuwa kwenye muundo wa MCQs na kusisitiza watoto inabid wakokotoe...! Watanzania bhana kwa unafiki hatujambo
 
Leo mnasifia MCQs za vyuo vikuu wakat huo huo mnaponda utaratibu wa mitihan ya darasa la saba kuwa kwenye muundo wa MCQs na kusisitiza watoto inabid wakokotoe...! Watanzania bhana kwa unafiki hatujambo

Mambo haya ni ya kuiga ili angalau tusogee ulimwengu wa tatu, sasa kama watu mna njia za mkato pendekeza, haya mambo ni ya kitaalamu zaidi.
 
Unaambia Yote Ni Majibu Ila Kuna Moja Ni Sahihi Zaidi
 
Teh Teh vyuo vya siku hizi ni kuzalisha vilaza tuu...Teh Teh..Kuna mtu aliniambia hata UDOM wanatumia mtindo huu!

Mnayo kazi sana...hiyo inaitwa voda fasta...
 

Huu upuuzi wa mutiple choice naupinga kwa kila level...huu ni ujinga tuu na uwezi kumpima mtu kwa multiple choice..huu mtindo umekuja baada miaka hii baada ya idadi ya wanafunzi vyuoni kuanza kuongezeka kwa hiyo hapo lengo ni kulinda muda wa kusahahisha maswali..na wanaona uvivu maana wanafunzi ni wengi.

Multiple choice mtihani mzima ni upuuzi wa aina yake na una zalisha watu wasio elewa mambo bali wabahatishaji ndio maana unaweza kuta mtu kafaulu kumbe kapiga chabo na kichwani mtu...
 
Bora ukutane na essay kuliko mcq...udsm ni chuo kigumu sana ikifuatia na mzumbe,tia pamoja dit.


Kwamba umesoma kote huko ndio maana unajua ugumu wa vyuo vyote hivyo

Unaijua Medical School?
 
Watanzania tutazidi kuburuzwa, we Unang'ang'ania kitumike kipimo chako cha kuiga unajua kitakachopimwa? Acha watu watoke, na kwa sasa hatuwezi kubadili kule juu -Ushauri wenu ungefaa kujenga uwezo kuanzia elimu ngazi za chini.
 

Ajabu sana inawezekana hujui lolote nini maana ya mtihani cha mno ni level of understanding.Nilikuwa Muce lakini kuna test Fulani darasa la watu 900 wa kwanza alikuwa na 12 out of 20 wengi sana zero mpaka tano.GPA udsm huwezi pata ya tano hebu uliza st Joseph na sauti kwenye essay kama za darasa la awali hadi aibu.Gpa hadi za tano.Udsm tunaoondoka na GPA chini ya 3.5 ndo kibao lakini wenzetu wengi wanatoka na zaidi ya 3.5
 
secondar na chuo ni vitu viwili tofauti mcqs za chuo zinahtaji mtu uelewe vizuri consept ndo unaweza kupata,maana majibu yote ni kweli lakini pale kuna kweli zaidi, ukitaka kujua hilo kutana na dr Ananda pale udom
 


ni sahihi usemacho mkuu kwa upande wa saut gpa za 3.5 ni nyng sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…