KUULIZA SI UJINGA

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
3,359
Reaction score
4,528
Habari zenu wanajukwaa natumai mpo poa, nami nipo vyema kiafya namshukuru Mungu siku imeenda vyema. Hadi Wikiendi hiyo imegonga hodi fasta, kama injini ya tumbo la kuendesha.

Lengo la kuileta kuandika haya maneno limelalia kwenye msamiati usiyo rasmi mpya ambao niliuona ukivuma sana mtandaoni. Imekuwaje ukazuka akabambikiziwa mtu likawa ni jina. Ni hili neno PUGI.

Miaka mingi nyuma kipindi nipo shule ya msingi nilitokea kuwa mfugaji njiwa mzuri. Ambapo nilikuwa nao wa porini wa kufungiwa kwenye tundu na pia wa kawaida wa kuachiwa wajiendee na kisha hurudi.

Basi kipindi hiko njiwa wa kawaida tuliwaita MBUTA na njiwa pori ambao wengi wenu mnawajua kwa jina la TETERE tulipenda kuwaita PUGI.

Sasa ghafla bin vuu! Nasikia PUGI kuna watu wametunukiwa jina hilo. Ni kwa kigezo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…