Francisco mafwa
New Member
- May 5, 2024
- 1
- 0
Ukatali wa kijinsia; Ni kitendo chochote anachofanyiwa mtu kutokana na jinsi yake au majukumu yake ya kijinsia. Kitendo hicho ni kile ambacho kinaweza kumuathiri mtu kimwili, kiakili, kijinsia au kisaikolojia.
Miaka ya nyuma ilizoeleka kuwa ukatili wa kijinsia wanafanyiwa wanawake na watoto tu, lakini sasa hivi tunashuhudia wanaume nao wamekuwa wakikabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia.
Ukatili unaweza kuwa ukatili wa kingono mfano kubakwa. ukatili wa kimwili mfano vipigo, shambulio la mwili, kuchomwa mwili na moto au ncha kali, matumizi ya silaha, kuvuta nywele, kusukuma au ukatili wowote mwingine.
Ukatili wa kihisia/kisaikolojia mfano matusi kwa njia ya maneno au ishara yenye lengo la kudhalilisha, vitisho na kutishia kufanya fujo, maneno ya kufedhehesha, kudharauliwa hadharani, kutishia kutoa siri, kuingiliwa faragha, kutishiwa kuuawa, wivu wa kupindukia,kunyang’anywa watoto kwa makusudi n.k. Ukatili wa kimwili una madhara mengi kama vile majeraha, ulemavu na wakati mwingine hupelekea hadi kifo.
Ili kuipata Tanzania iliyo bora lazima serikali iunde Tume ya kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia na hii ni kutokana na kuwepo kwa mfululizo wa matukio ya ukatili wa kijinsia nchini. Tumekuwa tukishuhudia kuwepo kwa tume mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwemo TAKUKURU, NEMC, Tume huru ya uchaguzi.
Ili kuweza kuunda tume ya kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia taasisi zifuatazo zinatakiwa kujumuishwa kwenye Tume.
I) Serikali yenyewe; Uongozi wa tume unakuwa uanzie serikali kuu hadi serikali za mitaa ambazo ni mkoa, halmashauri, kata, kijiji na mitaa. Hii itasaidia kupata taarifa za ukatili kwa uharaka na kulifanyia utatuzi.
Il) Taasisi za kidini; Masheikh na Mapadri wanatakiwa kujumuishwa kwenye tume ili kuwawezesha na kuwapatia waumini na wafuasi wao elimu kuhusiana na ukatili wa kijinsia. Hii itawafanya waumini kuwa na hofu ya Mungu.
Ill) Taasisi za afya; Hii taasisi itakuwa na wajibu wa kuwahudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia ikiwemo kuwatibu kimwili na kisaikolojia ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ukatili waliofanyiwa.
IV) Taasisi za ulinzi na usalama; Jeshi la polisi linatakiwa kuwepo kwenye tume ili kuwajibika kuwakamata wahusika wa matukio ya ukatili. Pia litakuwa na wajibu wa kumlinda muathirika wa unyanyasaji dhidi ya mshukiwa wa tukio na pia kumfanya muathirika asijichukulie maamuzi mengine ikiwepo kujiua.
V) Mahakama; Mamlaka za kisheria ndio zitakazokuwa na wajibu wa kutunga, kutafsiri na kutoa hukumu kwa watuhumiwa watakao bainika kuhusika katika vitendo vya ukatili wa kijinsia kulingana na ushahidi utakaotolewa na kusimamia vyema sheria zilizotungwa.
Vl) Taasisi za elimu; Ili kuhakikisha ilimu inatolewa ikiwemo elimu rasmi na isiyokuwa rasmi lazima taasisi za elimu zihusishwe ili kutoa elimu mashuleni na katika jamii.
Vll) Mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia; Hizi nazo zitawajibika katika kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia katika eneo husika ikiwa ni kwa kutoa elimu, kusimamia kesi za ukatili wa kijinsia, na kuilinda jamii na wahanga wa matukio ya ukatili.
Ili kupambana na ukatili wa kijinsia maeneo yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa;
i) Kuimarisha Uchumi wa Kaya; uchumi wa kaya mbalimbali unatakiwa kuimarishwa ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu pia kuingizwa kwenye mfumo wa kunusuru kaya maskini yaani TASAF.
ii) Mila na Desturi; Mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia kupigwa marufuku ikiwemo ukeketaji, Jando na unyago na sherehe zingine za kitamaduni zinazofanyika katika jamii zetu hasa zile zinazofanyika wakati wa mavuno pia zinatakiwa kupigwa marufuku kwa sababu nazo huchangia kutokea kwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo wasichana kulazimisha kufanya mapenzi na hata kubakwa.
iii) Mazingira Salama; Serikali inatakiwa kuhakikisha usalama kila mahali ikiwemo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mashuleni, kwenye huduma za afya, na maandishi ambayo jamii inaishi.
iv) Malezi, kuimarisha mahusiano na kuziwezesha familia; Wazazi wanatakiwa kuhimizwa na kuwajibika katika malezi na makuzi sahihi ya watoto wao na kuwa karibu na familia zao ili kuweza kutambua mapema changamoto ambazo zitajitokeza ikiwemo watoto kufanyiwa ukatili au watumishi wengine.
v) Utekelezaji na usimamizi wa sheria; Sheria zilizowekwa za kumuajibisha mtuhumiwa wa ukataili wa kijinsia zinapaswa kutekelezwa kama zilivyo ainishwa na kusimamiwa kwa ukaribu sana ili kusiwepo na dhuruma
vi) Utoaji huduma kwa waathirika wa ukatili; Mfano ushauri wa kisaikolojia. Waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia wanatakiwa kupewa huduma ya ukaribu ili kuepusha muathirika kujichukulia maamuzi yasiyo kuwa sahihi ikiwemo kujinyonga.
vii) Uratibu, Ufuatiliaji na Tathimini; Time lazima ufuatilie muenendo wa kesi zote za unyanyasaji wa kijinsia na kufanya tathmini ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.
Hitimisho, ili kuweza kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini, lazima tuwajibike, tukubali kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati hata kama kutatokea tofauti katika jamii zetu, na kutoa taarifa zinazohusiana na ukatili wa kijinsia katika uongozi na sehemu husika. Ni lazima " tukubali tofauti zetu kwenye familia; kuimarisha malezi ya watoto".

Upvote
2