Kuunganisha DR Congo na Tanzania

Kuunganisha DR Congo na Tanzania

DEO G

Member
Joined
Mar 27, 2007
Posts
11
Reaction score
2
Naomba kujua hii serikali ya sasa inaendeleaje na mkakati wa kuunganisha DR Congo na Tanzania Ili mizigo ya DR Congo isipitie Zambia bali ipitie Tanzania na kufika DR Congo kupitia Sumbawanga
 
Naomba kujua hii serikali ya sasa inaendeleaje na mkakati wa kuunganisha DR Congo na Tanzania Ili mizigo ya DR Congo isipitie Zambia Bali ipitie Tanzania na kufika DR Congo kupitia Sumbawanga
Serikali ya nchu hii ni kichwa cha mwendawazimu bro..Mimi na elimu yangu ya pangu pakavu kichwani nina plan kibao ambazo kutokana na Rasilimali zilizopo nchi hii zinaweza kurahisisha suala la usfirishaji wa mizigo kiurahisi kwenda Congo..lakini huwezi kuta wanauchumi wanajadili hiki kitu pamoja na kwamba Congo drc ni mdau mkubwa sana katika kuimarisha uchumi wa nchi hii
 
Naomba kujua hii serikali ya sasa inaendeleaje na mkakati wa kuunganisha DR Congo na Tanzania Ili mizigo ya DR Congo isipitie Zambia bali ipitie Tanzania na kufika DR Congo kupitia Sumbawanga
Acha porojo zisizo na msingi,jiografia ipi hiyo itakayofanya mizigo ya kwenda Lubumbashi ipite Sumbawanga?

Huu uzushi sijui nani aliwadanganyaga.
 
Okay wacha nikueleweshe plan ya america walitoa hela kutengeneza lami ya tdm sumbawanga then kasanga! Huko kote tumejenga imebaki km chache matai to kasanga port, pale ilitakiwa iwe ferries za maana kuvuka ziwa halafu upande wa Kongo nao wapige lami mpaka Lubumbashi!
Sasa kilichotokea upande wetu tumefanya vizuri mno cause tumebaki na kama km 30/40 tuu sasa ba Kongo aisee walikula hela hawajafanya lolote! Kwao ilitakiwa watengeneze km kama 500 hivi sasa jamaa hata km Moja hawajatengeneza!
 
Kasanga and Kalema...perfect targets ...Kalemie DRC ipo reli inayo fyonza Congo Mashariki na Magharibi
 
Inategemea mzigo unaupeleka sehemu gani ndani ya Jamhuri ya Congo. Kwa Lubumbashi njia ya reli ya TAZARA na barabara kupitia border ya Tunduma ndio suruhisho.
Kwa mzigo unaolenga kufika mikoa ya katikati ya DRC hadi Kinshasa, njia itakayofaa siku za usoni ni hii ya Katavi - Karema hadi Kalemie na baadaye kwa reli upande wa DRC... Ingawa siyo ya uhakika sana.
Kwa mzigo unaoenda Uvira na kaskazini mwa DRC kuna njia tatu: kwanza ni Reli hadi bandari ya Kigoma na kusafirisha mzigo kwa meli za mizigo hadi Bujumbura, na kuendelea kupitia Uvira au kusafiri hadi border ya Ruhwa upande wa Burundi, na kusafiri kuitafuta Bukavu DRC au Cyangugu aidha kwa meli hadi Goma.
Njia nyingine mbili za kuaminika, ni kupitia Kasulu kwenye border ya manyovu, Makamba, Gitega hadi Goma au njia iliyozoeleka ya Rusumo, Kigali, Goma hadi Kisangani.
Tatizo la DRC ni ukubwa wa nchi isiyo na miundombinu bora ya barabara ambapo usafiri pekee unaoaminika kwa mizigo ni maroli tena mengi yaliyochakaa.
 
Vyote 2 ni Vijijini,Bora tungekaza njia ya kwenda Goma,Butembo,Uvira nk ila sio hivyo Vijijini umevitaja hakuna kitu huko
Ni vijiji vya wapi nimetaja? Muunganiko wa Karema na Kelemie unaujue vizuri?

Unajua potential ya hayo maeneo kama yakitukiwa effectively according to geographical Locations?
 
Sio kupitia Sumbawanga ni kupitia Katavi bandari ya Karema.

Bandari ya Karema imeshakamilika kwa sasa
Kuna bandari ya Kipiri haifanyi kazi yoyote ,kirando ni kiungo muhimu Sana kwa mizigo ya kongo(Moba) kupitia pale kwenda kipiri na kwenda kongo kuliko kutumia karema ambapo ni mbali Sana na wakati huo kuna bandari ya kabwe.
 
Naomba kujua hii serikali ya sasa inaendeleaje na mkakati wa kuunganisha DR Congo na Tanzania Ili mizigo ya DR Congo isipitie Zambia bali ipitie Tanzania na kufika DR Congo kupitia Sumbawanga
EeeeenHeeee Heeee! Malindi Kenya hadi Bagamoyo

Mkuu 'DEOG.' usinione hamnazo kwa hicho kicheko hapo juu!

Ngoja nikudokeze kwa mifano halisi, pengine itakufanya na wewe uone picha halisi ilivyo:

1. Kuna pesa tunakopeshwa na AfDB kujenga barabara inayoambaa ambaa kando ya Bahari ya Hindi toka Malindi, Kenya hadi Bagamoyo, Tanzania.

2. Kuna barabara nyingine muhimu sana kama hiyo niliyoitaja hapo juu, ambayo yenyewe itaunganisha Arusha na kuelekea Moshi hadi mpakani Holili/Taveta, Kenya. Hii barabara nzuri ipo, lakini inaboreshwa ili watumiaji wake wanufaike zaidi kwa biashara zetu hapa Afrika Mashariki.
Hapo Arusha, ni juzi tu imezinduliwa barabara inayochepukia Kusini mwa mji na kuungana na ile inayokwenda Kilimanjaro. Hii barabara ni muhimu zaidi kwa kuunganisha na Namanga, kuelekea Kenya; na zaidi ya yote, ni kwenye barabara hiyo inayozalisha ile inayoteremka hadi Singida na kushikana na ile inayokwenda Burundi, ili malori toka Mombasa yapitishe mizigo yao kiurahisi zaidi kuelekea huo Burundi, kwani Bandari yetu ya Dar es Saalam haina ufanisi mkubwa.

Kwa hiyo, kiufupi, bila shaka unaweza kuona mahali nguvu zetu zilipoelekezwa zaidi ya mahali kwingine kokote; na huko unakokuzungumzia wewe, bila shaka utaona hatuna msukumo nako.
Na siyo huko tu, bado hujaulizia Uganda je, hatuhitaji nako tukawa na usafiri mzuri kuelekea huko?

Ngoja nikuache utafakari haya. Ukiwa na nguvu na hamu ya kujadili nitarudi kujadili nawe.

Lakini naomba unielewe, hicho kicheko kirefu kisikuhadae, ni kicheko cha maumivu na kuililia Tanzania yetu hii isiyojuwa inakwenda wapi!
 
Serikali ya nchu hii ni kichwa cha mwendawazimu bro..Mimi na elimu yangu ya pangu pakavu kichwani nina plan kibao ambazo kutokana na Rasilimali zilizopo nchi hii zinaweza kurahisisha suala la usfirishaji wa mizigo kiurahisi kwenda Congo..lakini huwezi kuta wanauchumi wanajadili hiki kitu pamoja na kwamba Congo drc ni mdau mkubwa sana katika kuimarisha uchumi wa nchi hii
Viongoz wengi wana feli hapo tu
 
Okay wacha nikueleweshe plan ya america walitoa hela kutengeneza lami ya tdm sumbawanga then kasanga! Huko kote tumejenga imebaki km chache matai to kasanga port, pale ilitakiwa iwe ferries za maana kuvuka ziwa halafu upande wa Kongo nao wapige lami mpaka Lubumbashi!
Sasa kilichotokea upande wetu tumefanya vizuri mno cause tumebaki na kama km 30/40 tuu sasa ba Kongo aisee walikula hela hawajafanya lolote! Kwao ilitakiwa watengeneze km kama 500 hivi sasa jamaa hata km Moja hawajatengeneza!
Mizigo ikianza kupita pale watatengeneza tu
 
Back
Top Bottom