Mimi nafikiri, kisheria kama una back ups za kutosha (e.g. wiring ilikuwa confirmed na TANESCO) and kama kweli tatizo ni uzembe wa Tanesco, kwa mfano kuungua kwa Transformer au kuanguka kwa nguzo, hapo, lazima ulipwe. And I think watanzania tumekuwa wapole sana ndio maana hata hawa Tanesco wamekuwa wakituchezea sana.
Kwa upande mwingine, kuna maeneo kwa mfano Makumbusho Dar es Salaam, huko kuna transformer moja linaitwa kwa mateja. Halooo, jamaa wanaotumia hili transformer, kuna msimu huwa wanakoma kabisa. Inaweza kufululiza wiki nzima ikifika saa tatu tu, umeme unakatika. Yaani kuna mkazi wa huko aliwahi kuniambia, hawa jamaa wanajua kuna kitu kinacholeta shoti but they are leaving it, ili wapate overtime. Hili transformer limekuwa likipata shoti mara kwa mara, and Tanesco wana taarifa kamili as umeme ukikatika tu, mtu akapiga simu na kusema anatoka makumbusho, utasikia tu, "ni transformer la mateja". Sasa kama Tanesco wanajua kuwa hili transformer ni feki, and they are entertaining it, siku makumbusho ikigeuka makaa kwa nyumba kuungua, wewe unafikiri Tanesco kisheria hawatakuwa held responsible kweli...??
Nchi zilizoendelea, naamini umeme hata ukikatika kwa masaa machache ndani ya siku 365, basi hapo claims zitakuwa za kumwaga. Bongo, wanakata wanawasha, wanachezesha mpaka TV za walalahoi na wasio walalahoi, zinaungua, but hakuna anayeclaim. I think, watanzania tuunganishe nguvu na kuanza kuwabana hawa watu. Tanesco inaishi kwa kodi zetu, and on top of that, tunawalipa kwa huduma za umeme, then wanatuchezea shere. They must be held responsible.