Pole sana kwa kuwa sheria zetu ni copy/cut and paste, vyuoni ilijulikana kama ku-cram au kumeza, itabidi hapa tuangalie sana waingereza idara yao ya nishati inasemaje wanapokuwa na case kama hizo zinazotokea Tanzania na haswa zikisababishwa na TANESCO the "rabid" company
Pole kwa kupoteza mali zako kwa namna hiyo uliyotaja,,,,,sawa kopi au pesti lakini na sisi pia tunasheria kama hizo hasa katika sheria ya madhara (law of tort) na kama tanesco wanakata umeme ni lazima watoe taarifa kwa kila mdau au kupitia magazeti au vyombo vingine kama tv na redio nk
Kama uliunguliwa na ilihali ikiwepo taarifa kutoka tanesco na kwa kutojali ukaacha jokofu kwenye umeme itakuwa ngumu kulipwa.
Na lazima kwenye shitaka uoneshe wajibu wa tanesco kwa mteja ikiwa ni pamoja na kutoa habari
pia uoneshe kuvunjwa kwa wajibu yaana kutotoa habari kwa mteja na
pia uoneshe madhara uliyoyapata ikiwa ni kuunguliwa kwa jokofu
case laws donoghue v.stevenson , benson bezibwa v.cocacola kwanza ltd etc alafu tukikosa kabisa kwetu tunaenda katika JALA s.2(2)
Kuna declaration forms ambazo ni sehemu ya mkataba na TANESCO. Kuna haja ya kuliangalia hilis suala upya na kuleta sheria zitakazomlinda mtumiaji. Sera na sheria zilizoanzisha TANESCO zimepitwa na wakati.
My Take: to avoid the hasle of the legal system...make sure you insure your properties. It is cheap and more secure than the path to sue TANESCO which is not a guarantee to succeed.
Mkuu S,
Hao insurance wa Tanzania wanaeleweka? Kuna jamaa yangu alipata matatizo ya kuunguliwa na gari lake ambalo aliliwekea comprehensive insurance. Huwezi kuamini aliombwa atoe pesa ili wamsaidie. Sasa hapo kuna kitu kweli? Umepata hasara halafu unatakiwa kutoa pesa nyingine!
Ahsante mkuu B na pole sana ndugu yetu SteveD. Maelezo hapo juu ni mazuri sana ila kuna mtu aliniambia kuwa kwa hali ya Tz inakuwa ngumu kuwashitaki Tanesco. Kama sikosei, nakumbuka kuwa kuna suala la uwekaji umeme (electrical installation) ambalo jamaa wanatumia kukwepa kulipa fidia. Alinambia kuwa inabidi mambo ya kufunga nyaya na vitu vyote vya ndani yawe yamepitiwa na wataalamu wa Tanesco na kukubaliwa. Sina hakika lakini kama hiyo kweli basi uwezekano wa kulipwa ni mdogo sana endapo ufungaji wa nyaya ulifanywa na mafundi wetu wa mitaani kama wengi tunavyofanya. Yaani kuna kitu zaidi ambacho hawa jamaa hawaweki wazi ila wanakitumia kuruka viunzi.
Kuna declaration forms ambazo ni sehemu ya mkataba na TANESCO. Kuna haja ya kuliangalia hilis suala upya na kuleta sheria zitakazomlinda mtumiaji. Sera na sheria zilizoanzisha TANESCO zimepitwa na wakati.
My Take: to avoid the hasle of the legal system...make sure you insure your properties. It is cheap and more secure than the path to sue TANESCO which is not a guarantee to succeed.
Kishazi, ile siku tunaunguliwa wala hatukupata chance ya kuzima swichi. Ni kawaida kwamba kila pale umeme unapokatika, tunahakikisha vyombo vyote vya ndani vinakuwa vimezimwa mara moja. Lakini siku hiyo ile tunakimbilia kuzima tu umeme huo umesharudi tena kwa fujo na kuunguza hivi vifaa. Mimi nadhani kuna fundi mmoja alikuwa sehemu sehemu kwenye mamitambo yao ambayo alitakiwa akate umeme pahala lakini akajikuta amekata sehemu isiyo na kuamua kurudisha umeme bila kufata taratibu.
Kuna ndugu mmoja nimeongea naye amesema wao nyakati za nyuma waliunguliwa na nyumba kabisa, na hamna fidia waliyofanikisha kuipata. Tuungane kuwabana Tanesco, wamezidi.
Ahsante mkuu B na pole sana ndugu yetu SteveD. Maelezo hapo juu ni mazuri sana ila kuna mtu aliniambia kuwa kwa hali ya Tz inakuwa ngumu kuwashitaki Tanesco. Kama sikosei, nakumbuka kuwa kuna suala la uwekaji umeme (electrical installation) ambalo jamaa wanatumia kukwepa kulipa fidia. Alinambia kuwa inabidi mambo ya kufunga nyaya na vitu vyote vya ndani yawe yamepitiwa na wataalamu wa Tanesco na kukubaliwa. Sina hakika lakini kama hiyo kweli basi uwezekano wa kulipwa ni mdogo sana endapo ufungaji wa nyaya ulifanywa na mafundi wetu wa mitaani kama wengi tunavyofanya. Yaani kuna kitu zaidi ambacho hawa jamaa hawaweki wazi ila wanakitumia kuruka viunzi.
Tanesco hawako liable for anything other than matatizo ya transformer yao, au kudondoka kwa nguzo yao. ukileta vifaa chakavu kwenye nyumba yako, watakusumbua sana kwenye fidia. tumeona wengi wamekosa hilo. labda kwasababu sheria haina upande wa shilingi, inategemeana, pengine kesi yako wewe ndo itakuwa landmark ya kwanza, kuweka msimamo huo hapa tz, ila kwa kipindi cha nyuma, fidia hiyo ni ngumu kupata na mara nyingi hutapata labda kwa hayo niliyosema hapo juu. tuwe makini na mafundi vishoka, nyaya za kichina nk.bidhaa bandia na vitu vya bei rahisi ambavyo tunavipenda ndo tatizo hapa.