Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kati wa watu wanaothamini sana uhai wa watu wao hapa duniani ni Israel. Ikitokea raia wa Israel au Mwanajeshi wa Israel amefariki kwenye mapigano au tukio lolote lile la Kigaidi haijalishi inapita muda gani, Israel ni lazima walipize kuuliwa kwa mtu wao.
Tabia hii ya Israel inapekea sio tu kuheshimiwa na mahasimu wao bali kuogopewa sana duniani katika medani za intelejensia na vita. Shirika lao la Ujasusi (MOSSAD) pamoja na vikosi vya jeshi lao wanafahamika sana kwa kutekeleza mission mbalimbali kwa ajili kulipiza vifo vya watu wao ili kutuma ujumbe kuwa wao sio watu wa kawaida.
Sote tumesikia kuwa Wanajeshi wetu 2 wameuwawa huko Congo pamoja na wengine 25 kujeruhiwa. Mauaji hayo yamefanywa na wanamgambo wa M23 ambao wanaungwa mkono na Rwanda.
Mbaya zaidi tumesikia kuwa Rwanda imefanya vitendo vya kuwadhalilisha kisaikolojia wanajeshi wetu wakati wanavuka mpaka wakiwa na Wanajeshi wa SADC ambao pia wamejeruhiwa kwa kuwachelewesha masaa kadhaa mpakani.
Baada ya matukio haya ambao sio tu yameliumiza Jeshi letu bali Watanzania wote tunaoipenda na kuijali kweli nchi yetu, Swali langu ni Je, kuna haja kwa Shirika letu la Ujasusi na Jeshi letu kulipa kisasi kutokana na mauaji na kujeruhiwa kwa ndugu zetu kama wanavyofanya Mossad na IDF?
Hawaoni kuna haja ya kufanya hivyo au ndo tumeshakubali rasmi sasa kuwa Rwanda ndo mtabe wa Afrika kwamba tumemshindwa na wanaomuweza ni Wazungu tu?