Citizen Kane II
New Member
- Jun 21, 2024
- 2
- 2
Kuuza Hewa kumaliza tatizo la Upungufu wa ajira Kwa vijana angalau 10%
Katika andiko hili ninakwenda kuelezea kuhusu uuzaji wa hewa, kunakohusiana na kufanyika Kwa shughuri zinazohusisha kupunguza au kufyonza hewa ya ukaa inayotokana na shughuli za kibanadamu kama vile viwanda, usafirishaji na uzalishaji nishati.
Katika andiko hili nitaelezea namna mashirika au kampuni binafsi zinavyofaidika na uuzaji wa hewa Kwa makampuni ya kibepari.
Pia nitaelezea jinsi makampuni haya yalivyowekeza Tanzania. Pia nitaelezea jinsi gani tatizo la ukosefu wa ajira Kwa vijana nchini Tanzania ni kubwa na jinsi serikali inavyoweza kutatua Kwa kiasi Kwa kuwapa nafasi vijana kuuza hewa Kwa makampuni yanayozalisha gesi ya ukaa, nitatoa mfano wa jamii ambazo zimefaidika Moja kwa Moja Kwa kuwapa wananchi wa kawaida nafasi ya kuuza hewa.
Kwa kumalizia nitatoa ushauri namna serikali inavyoweza kuachana na wawekezaji wa nje na kuwashika mkono vijana waweze kuvuna na kuuza hewa na kupiga ndege watatu Kwa jiwe Moja yaani kupunguza ukosefu wa ajira Kwa vijana, kuingiza kipato na fedha za kigeni na wakati huo huo kutunza mazingira.
Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030 soko la huwa ya ukaa linaweza fikia thamani ya zaidi ya Dola za kimarekani bilioni 40 ikiwa Bei ya Hewa ya Kaboni itafikia Dola za kimarekani 80 Kwa kila tani ya hewa ya ukaa.
Na Kwa makadirio hayo uuzaji huu wa hewa ya ukaa utazalisha zaidi ya kazi milioni 190 barani Afrika (kulingana na jarida la Africa Renewal toleo la Mei 2024).
Na inawezekana soko hilo likapanda thamani hadi kufikia Dola za kimarekani tilioni moja na bei ya hewa ya Kaboni kufikia zaidi ya Dola za kimarekani 200 iwapo juhudi za kimakusudi zinazofanywa na mashirika ya kimazingira duniani zitafanikiwa.
Kwa Sasa bei ya hewa ya Kaboni Kwa tani inatofautiana kutoka Nchi Moja kwenda nyingine ikianzia Dola za Kimarekani 12 hadi 40.
Biashara ya kuuza hewa ya ukaa ni Nini? Na hufanyikaje? Biashara ya kuuza hewa ya ukaa ni biashara kama biashara nyingine kwa kuwa biashara hii ina tabia au inaundwa na tabia zile zile ziundazo biashara nyingine.
Tabia hizo ni kuwepo Kwa Mnunuzi au Hitaji la bidhaa(demand Kwa lugha ya kiingereza), pia Kuna Msambazaji au usambazaji(supplier, supply) pia Kuna Bei/thamani ya bidhaa(price) na pia biashara hii ina masoko yake.
Katika biashara hii ya uuzaji wa hewa ya ukaa Wanunuzi wakuu au wahitaji ni makampuni makubwa wazalishaji wa hewa ya ukaa, mataifa makubwa yaliyoendelea katika uzalishaji wa nishati zinazozalisha Kwa kiasi kikubwa hewa hii ya ukaa, Mataifa haya hununua kila tani ya hewa ya ukaa Kwa maana hii, Kwa kila tani ya hewa ya ukaa wanayozalisha hutoa au hugharamia Kwa kutoa kiasi fulani cha pesa ili kufidia au kugharamia miradi ya kimazingira au shughuli zinazofanywa kokote kule duniani ili kupunguza/kuzuia uzalishaji wa hewa ya ukaa mfano matumizi ya nishati mbadala zinazozalisha hewa ya ukaa kidogo mfano matumizi ya majiko banifu au biogesi au shughuri zinazohusisha kuwezesha asili kufyonza kila tani ya hewa ya ukaa inayozalishwa mfano upandaji wa miti na utunzaji wa misitu ya asili.
Kwa ufupi ni kuwa ili makampuni haya yapate kibali Cha uzalishaji basi ikiwa yamechafua au yamezalisha tani elfu Moja za hewa ya ukaa basi ni lazima yanunue tani elfu Moja ya hewa ya ukaa katika masoko ili yaweze kupata kibali cha uzalishaji.
Kwa Sasa Kuna masoko mawili yanayohusika na uuzaji na ununuaji wa hewa ya ukaa masoko hayo hujulikana Kwa Soko la hiari la hewa ya ukaa(Voluntary Carbon Market VCM) Soko hili ni la hiari kama jina lake lilivyo yaani ina maana mtu yeyote anaweza kuuza na kununua.
Soko linguine ni Soko la Masharti la hewa ya ukaa (compliance or regulated carbon market) katika Soko hili makampuni hubanwa serikali kununua hewa ya ukaa kulingana na uzalishaji wa hewa hiyo katika Soko hili serikali za Nchi husika ndizo huwa na amri ya kuamua makampuni yanunue kiasi gani cha hewa ili waendelee na uzalishaji.
Tanzania ni Moja ya Nchi wafaidika wa uuzaji wa hewa ya ukaa, februari 9 mwaka 2024 Waziri anayehusika na masuala ya muungano alisema kuwa mpaka mwezi huo kulikuwa na makampuni zaidi ya 39 yaliyokuwa yamesajiliwa Kwa ajili ya shughuli za uuzaji wa hewa ya ukaa ilhali ni makampuni 12 ndiyo yalikuwa tayari yameanza shughuli hizo na serikali ilikuwa inakadiriwa kuvuna mapato ya dola za kimarekani bilioni Moja.
Tanzania Ina utajiri wa hekta milioni 48 za misitu ambayo inaweza kutumika katika shughuri za uuzaji hewa ya ukaa, ilihali makampuni haya mengi yakiwa ya kigeni mpaka Sasa yamepewa fursa ya Uwekezaji karibu hekta milioni 5.
Pamoja na Serikali kuona kuwa Kuna fursa katika uuzaji wa hewa ya ukaa, fursa ya kutengeneza mamilioni, kwanini inashindwa kutumia fursa hiyo kushirikisha makundi maalumu kama vijana au wanawake katika kujikwamua kiuchumi?
Katika andiko hili ninatoa wazo kuwa serikali ifanye juhudi maalumu kuwapa nafasi hasa Vijana katika kutumia rasilimali za misitu kufanya shughuri za uuzaji hewa.
Juhudi hizo ni pamoja na kufanya uchambuzi na tafiti jinsi gani vijana wanaweza kuunganishwa, kupewa Elimu na kuwezeshwa ili waweze kuvuna fursa hii.
Serikali inaweza kuwaunganisha wadau mbalimbali kama vile asasi na NGOs mbalimbali za kimazingira ili kuwawezesha vijana kiujuzi, kiteknolojia ushauri wa kitaalamu kama tu inavyofanyika katika nyanja nyingine kama vile katika kilimo, uvuvi na madini.
Pia serikali inaweza kuwadhamini vijana Hawa Kwa mikopo ambayo wataweza kufanya biashara hii Kwa viwango vinavyohitajika kimataifa.
Nchini Kenya mwaka 2002 kusini mwa Nchi hiyo katika Kijiji Cha Gazi na Makongeni kulianzishwa mradi wa kuuza hewa ya ukaa, mradi huu ulimilikiwa na wanavijiji wa vijiji hivi viwili na mradi huu ulihusu hasa utunzaji wa miti ya mikoko na ulikuwa na ukubwa wa hekta 117 tu.
Kufikia mwaka 2013 mradi ulikuwa na thamani ya kuuza hewa ya ukaa kiasi Cha tani 3000 Kwa mwaka Kwa muda wa miaka 10 yaani mpaka 2033 na Kwa thamani hiyo kila mwaka mradi huu ulikuwa una uwezo wa kuingiza Dola za kimarekani 130,000 (Tsh 364,000,000). Kwa Uwekezaji wa hekta 117 tu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba Januari 07, 2022 alieleza, “serikali yenu, tunajua tatizo la ajira na tutajitahidi kutengeneza fursa mbalimbali ili vijana wapate ajira.” Basi ni wakati wa serikali kutumia fursa hii ya uuzaji hewa ya ukaa kutatua tatizo la ajira Kwa vijana.

Upvote
5