Kuuza / kununua nyumba, viwanja kwa US$ in Tanzania?

Joined
Feb 10, 2014
Posts
62
Reaction score
18
Hivi ni kweli kabisa kwamba ni lazima viwanja au nyumba viuzwe hapa nchini Tanzania kwa US$ na siyo Shs?

Maeneo ya mbezi beach, masaki na yafananayo. Na je malipo ya pesa ya kigeni yana uhusiano gani na kuporomoka au kukua kwa uchumi wa nchi changa kama Tanzania?

Hili jambo naona limeshika kasi sana na sielewi faida yake ni ipi kwa nchi.

Tafadhali mwenye uelewa naomba msaada, na kama huelewi pita kimya.
 
Kutoka 1961 mpaka leo bado nchi ni changa tu, sijui lini itakua.
 
Watawala wamechagua kufumbia macho tu, hivyo ku-create demand ya dola wakati wanacho-export ni next to zero. Wanaachia malipo ya ada za shule, kodi za nyumba, watoa huduma huduma za kawaida kama mahoteli na maduka ya bidhaa. Wanaishia kufanya maisha yetu magumu, mshahara shilingi kodi ya nyumba ulipe kwa dola!
 
Tatizo makaratasi yetu ya madafu hayaeleweki, wewe kama ni mnunuzi mtakokotoa kwa exchange rate ya siku hiyo utamlipa kwa madafu kama kawaida, sioni ubaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…