Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Goita (Goiter) ni uvimbe unaotokea kwenye tezi ya thyroid inayopatikana sehemu ya mbele ya shingo.
Tezi hii yenye umbo linalofanana na kipepeo huzalisha homoni za T4 na T3 ambazo huhusika kwenye kuratibu mifumo mbalimbali ya mwili ikiwemo joto, mihemko ya mwili, mapigo ya moyo na mmeng’enyo wa chakula.
Upungufu wa madini joto (Iodine) ndiyo chanzo kikubwa cha kutokea kwa ugonjwa huu. Wakati huu, tezi za thyroid huongezeka ukubwa ili kufidia upungufu uliopo, jambo ambalo huifanya ivimbe.
Sababu zingine kama uwepo wa kiasi kingi au kichache sana cha homoni za thyroid, maambukizi kwenye tezi za thyroid, saratani na ujauzito zinaweza kusababisha kutokea kwa Goita.
Dalili zake-
Samaki wa baharini, maziwa pamoja na bidhaa zake, mayai pamoja na maini ya wanyama ni vyakula vyenye utajiri mkubwa wa madini joto (Iodine)
Aidha, hakikisha kila siku unapika chakula chako kwa kutumia chumvi iliyo ongezewa madini joto (Iodine) ili ujiweke salama. Unaweza kuitambua chumvi yenye madini haya kwa kusoma kifungashio chake kwanza kabla haujainunua.
Tiba ya tatizo hii ipo, mgonjwa anapaswa kufika hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.
Chanzo: Cleveland Clinic

- Uvimbe shingoni
- Maumivu na Kukaza kwa shingo
- Ugumu kwenye kupumua na kumeza chakula
- Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
- Uchovu usio na sababu
- Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi
- Sauti kuwa ya mikwaruzo
- Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono yake juu