Kuvimba mashavu

Kuvimba mashavu

Suzzie

Member
Joined
Feb 25, 2009
Posts
98
Reaction score
12
Naombeni nisaidieni, mtoto wangu alivimba shavu la kushoto last week, uvimbe huo huanzia kwenye sikikio kushuka chini. nikampeleka hospital na akapewa ampiclox akapona, leo asubuhi kaamka kavimba upande mwingine na hata kula hawezi, je huo ni ugonjwa gani? unasababishwa na nini? na nini tiba yake? nimeambiwa shuleni kwao watoto sita wamepata hilo tatizo. tafadhali nisaidieni.
 
Inaonekana kijana wako amepata maambukizi ya aina fulani ya virusi vinavyoleta shida katika vifuko vya mate kwa jina lingine hitwa MATUKU au kwa kiingereza huitwa MUMPS.

Sio hali ya kutisha sana inaelekea amepata maambukizo shuleni hasa kama aliweka mdomoni PENSELI au PEN ya rafiki yake au ndugu yake aliyeambukizwa hapo mwanzoni.
Dawa ulizopewa zitaweza kumsaidia,kutakuwa na homa za hapa na pale baada ya siku tatu au nne atakuwa vema tu na ataweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
Lakini kama kuna mtoto mwengine hapo nyumbani ujue anaweza kupata maambukizi na yeye vile vile

POLE SANA
 
Pole dada hata mimi niliwahi kushikwa zina homa sana hizo hasa mida ya jioni, lakini atapona tu, mara nyingi unaambukizwa kwa njia ya hewa.
 
Ndugu... jitahidi kupata ushauri zaidi kwa madaktari bingwa wa watoto maana ugonjwa huu japo hudharauliwa... una athari mbaya sana kwa watoto wa kiume maana huweza kuathiri via vya uzazi.
 
nawashukuru sana ndugu zangu kwa kunitoa wasiwasi, kwani nilisha anza kuchanganyikiwa.
je nnikamnunulie ampiclox tena? kwani aliyopewa dose yake iliisha, au nimuache tu?
 
Mh! hapo ndio nazidi kuchanganyikiwa, mtoto wangu ni wa kiume pia. ngoja niombe ruhusa niwahi kumpeleka kwa dr. Asante Veracity.
 
Dawa ya ugonjwa huo ni hiyo hiyo na unaambukiza kwa hewa kwani mtoto wangu aliugua na wengine wakafuata ikiwa ni pamoja na mimi. kuna maumivu makali hasa wakati wa kula au kunywa lakini akipata ampliclox hali hiyo huisha.
mpeleke hospitali kwani ni ugonjwa unaojulikana
 
Naombeni nisaidieni, mtoto wangu alivimba shavu la kushoto last week, uvimbe huo huanzia kwenye sikikio kushuka chini. nikampeleka hospital na akapewa ampiclox akapona, leo asubuhi kaamka kavimba upande mwingine na hata kula hawezi, je huo ni ugonjwa gani? unasababishwa na nini? na nini tiba yake? nimeambiwa shuleni kwao watoto sita wamepata hilo tatizo. tafadhali nisaidieni.
Mwanangu amepatwa na tatizo kama hilo, lakini baada ya kumpatia dawa tajwa hapo juu alipumzika kama saa moja hivi akaanza kutapika, Je tatizo litakuwa ni nini?
 
Jamani shavu langu la kushoto linanepeana tu, utadhani nimeficha kitu Shavuni. Nini shida na Tiba.
 
Back
Top Bottom