Kuvunja Ungo

Kuvunja Ungo

fakalava

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2015
Posts
4,459
Reaction score
6,027
Habari za siku tele marafiki!
Baada ya kuwa nje ya Jf kwa muda leo nimepata wasaa kuwa nanyi tena.

Ni hivi... Majuzi nimekutana na rafiki yangu wa zamani ambaye tumekuwa wote tukasoma wote Primary na Secondary, alikuwa mtundu sana na mbabe.
Katika akanieleza visa vya kibabe vya kutumia nguvu ambavyo amewai kuvifanya.
  1. Kukunja nondo ya 16mm.
  2. Kubeba gunia la mahindi 140 kgs.
  3. Kukatiza kwa kuogelea kwenye mto wenye mamba.
  4. Gari yake ndogo Suzuki-Swift ikikwama kwenye matope huwa anaiinua na kuisogeza pembeni peke yake.
Kwa ujumla orodha ilikuwa ndefu, baadaye nikamuuliza "Umewahi kuvunja Ungo?"
Ghafla jamaa akawa mkali- "hacha masikhara bwana, siwezi kuvunja ungo, ungo wanavunja wanawake.
Baada ya kuona jamaa kakasirika mimi nikaondoka zangu.

Hongera wanawake mnazo nguvu za kuvunja vitu ambavyo wanaume hawawezi kuvunja.
 
Baada ya kukaa mda mrefu, umekuja na huu uzi... Chit chat
....
 
Back
Top Bottom