Kuvunja utata kwa wanaosema ule mwezi ni wa jana.

Kuvunja utata kwa wanaosema ule mwezi ni wa jana.

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Katika mambo yanayonishangaza ni hii kaulii ya kusema kuwa "ule wa jana kabisa ulee sio wa leo"

Wengine husema waleo hauwezi kuchelewa vilee ule mkubwa huutafuti.

Binafsi nafuata mwezi wa kimataifa lakini hii haimaanishi nikubali kila linalosemwa na wenzangu kuwaponda wa mwezi wa kitaifa.

Katika hoja ambazo hazina tija wanazotumia baadhi ya watu ati kusema ule sio wa leo.
.NI KWELI ULE MWEZI HAUKUWA WA LEO(JANA)

Lakini je wamekosea ?

Hawajakosea kwa sababu ya hadithi ifuatayo.

Mtume wa Allah asema "fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona(kuonekana) ikiwa mtazongwa na mawingu basi kamilisheni siku thelathini"

Katika hadthi hii mtume alisema "..mkizongwa na mawingu basi kamilisheni thelathini.."

Na wala mtume hakusema "mkizongwa na mawingu basi kadirieni kuwa ulionekana tu ila mawingu yamezuwia hivyo fungueni"

Mtume hakueema hivyo 👆👆

Kitendo cha mtume kusema mkizongwa na mawingu kamilisheni maana yake ni kuwa huwenda bila mawingu kuzonga tungeuwona,

lakini mtume hakusema tukadirie tu assume kama tumeuwona bi akasema tukamilishe.

Hii ina maana kuwa pengine mwezi uliandama na mawingu yakazuwia hivyo kesho kuna uwezekano ukaonekana mkubwa kwa sababu pengine uliandama tokea jana ila tu mawingu yalizuwia kuonekana.

Na mtume kasema mawingu yakizuwia usijitie ku assume bali kamilisha thelathini.

Hivyo wanaosema kuwa ule mwezi haukuwa wa jana pengine ni kweli lakini mawingu yalizonga hivyo ikawa ngumu kuuona.

Kwa maana hii jana sikushangaa kuona mwezi ni mkubwa kwa sababu juzi kulikuwa na mawingu pengine uliandama ila kikwazo mawingu.

Binafsi nimefungua jana kwa rai ninayoiamini lakini suala la kukejeliana sio poa kwani hizi ni tofauti za rai enyi ndugu waumini.

Nawaomba tusherehekee kwa pamoja bila kukwazana kwa lolote.
 
Swala ni moja..wakat wanaanza kufunga waliona kua mwez ni wa siku moja nyuma...sasa walishindwa vip kufikiria kua siku zitakua zimetimia kwasababu wakat wanaanza walishakosea?binafsi nilianza nao ilawakat naanza niligundua nimekosea na nikasema ntafungua na waliotangulia kwakua niliona wako sahihi dhahir..na nikajua kabisa kua nadaiwa siku moja

Halafu hili swala limekua linajirudia karibia kila mwaka..je dini inatuzuia kutumia akili?ikiwa kwa miaka karibia mitano umekua unakosea kwa nini usijiongeze??
 
Hoja yako ni nzuri lakini napenda kukupa ushauri utambuwe kuwa mwezi katika Dunia yetu Upo mmoja.
 
Hoja yako ni nzuri lakini napenda kukupa ushauri utambuwe kuwa mwezi katika Dunia yetu Upo mmoja.

Ni kweli mwezi ni mmoja lakini ukija upande wa tarehe (Islamic calender) kila mmoja ana yake.

Mfano mzuri mara hii Saudi Arabia ilitangulia kufunga na kufungua na jirani yake Oman, hapo kila mmoja kafata mwezi wake.
 
Ni kweli mwezi ni mmoja lakini ukija upande wa tarehe (Islamic calender) kila mmoja ana yake.

Mfano mzuri mara hii Saudi Arabia ilitangulia kufunga na kufungua na jirani yake Oman, hapo kila mmoja kafata mwezi wake.
Kwa maana hyo kalenda za kiislam zipo tofaut.....!!? Niluyo nayo mimi inaniambia kuwa leo trh 14/05/2021 ni sawa na 02 Shawwal 1442, je kuna nyingne inasema leo n Shawwal 01......!!?
 
Hoja yako ni nzuri lakini napenda kukupa ushauri utambuwe kuwa mwezi katika Dunia yetu Upo mmoja.
Hoja sio mwezi tu usiishie kusema mwezi hoja ni mwezi MUANDAMO mkuu.

Ukisema mwezi tu ni jina pana,kuna mwezi ule mpevu mwezi masiku mwezi jina na mwezi muandamo.

Mwezi huu mpevu uko mmoja tu,lakini mwezi muandamo hauandami kwa watu wote.

Ishu hapa niwezi muandamo mkuu.

Ukiandama huku kule bado,ndio mwezi huu unaokusudiwa.
 
Back
Top Bottom