Kuvunjika kwa uchumba

Kijaaa

Member
Joined
Nov 19, 2017
Posts
26
Reaction score
37
Jamani wanasheria naombeni ushauri Mimi nilikuwa na mwanamke ambaye alikuwa mchumba wangu , na tulisha chumbiana mpaka kumvalisha Pete na mipango ya harusi ikaanza Sasa Basi akiwe yeye yupo katika hatua ya kujiandaa na send off na Mimi pia nikiwa najiandaa kwa harusi ambayo ilitakiwa ifanyike mwezi wa 9 ,lakini ajabu mwanamke amekuja kunitamkia kuwa tusitishe mahusiano yetu na hayupo tayari kuolewa na Mimi inshort hanitaki Tena , Sasa nauliza je Sheria inasemaje yanapotokea Haya

Naombeni ushauri na maana taratibu za kutaka mahali yetu irudishwe inaendelea lakini wazazi wa binti sio waungwana kila siku wanatupiga maneno tu , naombeni ushauri
 
Hapana kitu kama zawadi huwezi kudai hizo pesa pia kama ulitoa kwa hiari na sio mkopo huwezi kudai.. Sana sana labda udai fidia ya usumbufu navkupotezewa muda
Anhaaa nakuelewa Sana kaka nashukuru
 
Halafu kuna siku atalalamika kwamba shetani alimpitia anaomba mambo yaishe mrudiane....

Au atalalamika kwamba anamikosi ya kuolewa. Shenzi kabisa
Ni ngumu kuanza kumhukumu mapema kabla ya kusikia upande wake.. Mahusiano yanayofikia kipengele cha ndoa hukumbwa na mengi ya kutisha.

Nakumbuka mimi ile wiki ya harusi nilinusurika ajali mara 5, 2 zikiwa natembea kwa miguu na 3 nikiwa nadrive..kama nisingekuwa kamili leo hii nisingekuwa hapa
 
Uchumba mpaka kufikia hatua ya kutoleana mahari huwa umedumu kwa mda mrefu na mmeshajuana hadi tabia labda kama wameokotana chapchap
 
Si kila mmoja anaweza kupotezea kama wewe na sometimes mahari husika uliitoa kwa tabu kubwa...
 
Uchumba mpaka kufikia hatua ya kutoleana mahari huwa umedumu kwa mda mrefu na mmeshajuana hadi tabia labda kama wameokotana chapchap
Hizo dakika za lalasalama shetani husimamia show kwa namna ya ajabu kabisa... ! Nimeshakutana na kesi nyingi za namna hii na nyingine zikiwa ni simulizi za hapa JF
 
Dah broo nakuelewa Sana , yaani mpaka nahisi kafungwa kiakili maana akiulizwa kwanini umeamua anasema Mimi huwa namwambia njoo unifulie wakati bado hata ndoa sasa kiuhalisia haiingii akikini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…