Kuvunjwa kwa Baraza Mawiri Kenya. Hii itasaidia kitu gani?

Unao uhuru wa kujiandikia chochote... Lakini kumbuka 2008 siyo leo.
Na kesho itakuwa tofauti sana!
kumbe niko sahihi basi kwenye kwenye reply yangu,

ila kwa hisia zako ni kwamba waliokufa 2008 sio issue, ila waliokufa 2024 ndio wa maana sana, right?
 
Kupunguza pressure na ku balance ukabilaaa
 
Ni nchi ya watu wenye vichwa. Huenda baraza jipya ni sura mpya zote zenye uzalendo.
 
Kuongoza wakenya ni kazi kubwa sana, they aren't pushovers in every sense, simply wafanyie uliyowaahidi kwenye kampeni zako watakuunga mkono, lakini ukijaribu kwenda kinyume nao kazi unayo.

Ruto alikuwa na bahati sana ywa kuaminiwa na wakenya, bahati mbaya ameichezea wamemtingisha, sasa hata kama alikuwa na mpango wa kugombea muhula wa pili ajiangalie sana, hawamuamini tena.
 
Kupunguza pressure na ku balance ukabilaaa
Nadhani ni zaidi ya "kupunguza pressure."

Bwana Ruto aliona hatari kubwa iliyo kuwa inamnyemelea, hatari ya kuondolewa madarakani kwa nguvu. Sasa anafanya kila jitihada za kuepa janga hilo kwa kuwashirikisha wapinzani na kukubali kila kitu walichotaka Gen Z.

Bado haijulikani kama kweli amefanikiwa kuiondoa hatari hiyo moja kwa moja. Pengine atakuwa amefanikiwa kufunika tu kwa muda, itakapoibuka tena inamzoea kijumla.
 
Ndio kupunguza pressure kwa kusogeza mbele.......masmuzi hope pressure itashukaaas
 
It's more complicated than this.

Siamini kuwa Kenya walimwamini sana Ruto, hadi wakamchagua kuwa rais wao.

Ruto alijuwa tu namna ya kuyacheza makundi na makabila. Tokea alipo achana njia na rais wake Uhuru, alianza kampeni ya kuyashika makanisa. Kila Jumapili hakukosa kuwa katika kanisa fulani na kutoa harambee huko.
Akatumia mbinu ya kuwashawishi wakikuyu kuachana na Uhuru na rafiki yake mpya Raila, ambaye Kikuyu wengi walisha jiapiza hawezi kamwe kuwa rais wa Kenya, akafanikiwa.

Muungano wa Kikuyu na Kalenjini ni vigumu sana makabila mengine kuushinda.
Sasa hata Kikuyu wenyewe hawamtaki; hiyo ni hatari kubwa sana kwake.
 
" Sasa hata kikuyu wenyewe hawamtaki"

Hapo ndipo palinifanya niamini kama Ruto atathubutu kugombea tena, basi ana wakati mgumu sana.

Kwasababu nikitazama hata kwenye yale maandamano ya kumpinga, niliona mpaka yale maeneo aliyoungwa mkono wakati wa kampeni za kugombea Urais nao walimtosa, wakaamua kuungana wote wakenya kwa umoja wao kumkataa wakisema "Ruto umebadilika".

May be hii inaweza kuwa njia ya mwisho kwa Raila kuingia ikulu ya Nairobi, ajaribu kutumia kete ya kubadilika kwa Ruto na kupoteza imani kwa wakenya ili kuwaaminisha yeye atakuwa tofauti.

Hapa pia tuje kuona kama ukabila bado una nguvu Kenya au umeisha...
 
Ruto hakubadilika chochote mkuu 'denoo JG'. Ruto ni mtu 'cunning'; tapeli kwelikweli, tena 'ruthless' hasa.
Huyo jamaa, anafahamika toka enzi za KANU; akiwa kama akina Makonda wa hapa. Enzi za Moi ndio walikuwa vijana vinara wakijiita Youth for Kenya '92 (YK92), wakifanya kila aina za uchafu.

Huyo Bwana anasaidiwa sana na lugha ya ulaghai, wa kuwapumbaza watu, kama alivyo fanya kuwapumbaza "Huslers' na ile mikokoteni wakati wa kampeni zake. Ukimsikiliza leo kwenye huu mkasa unao mkabiri, lugha anayotumia ukimsikiliza kama ulikuwa hujui historia yake ya nyuma, itakuwia vigumu kutambua kwamba huyu mtu ni tapeli mkubwa sana.
Kwa bahati mbaya, Gen Z wamekwisha msoma vizuri, na hawaamini tena hiyo lugha tamu anayowauzia tena.
 
Aisee hiyo historia yake ndio umenipa leo, nilikuwa siifahamu kabisa, bahati nzuri Gen Z wameamua kumuadhibu kitendo cha kubadilika ametjiharibia sana imani aliyokuwa nayo kwa wapiga kura wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…