Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Kuvuta n'ge ili kufikia ulevi au to get high ni tatizo linalo kua kwa kasi katika ukanda wa kusini mwa Asia. Mojawapo ya nchi iliyo na matumizi makubwa ya ulevi huu ni Pakistan.
Ulevi au high hiyo inasemekana huwa maradufu zaidi kushinda heroine au cocaine, hudumu mwilini kwa zaidi ya masaa 10 hadi siku 3.
Mtumiaji hupitia maumivu makali kwa muda wa masaa yasiyo pungua sita baada ya kuvuta, kisha ndipo huanza kusikia ulevi au kuwa high.
Maumivu hayo huweza kupelekea kifo kwa mvutaji kwasababu chanzo kikuu cha ulevi huo ni sumu ambayo inapatikana katika maumbile ya n'ge.
MBINU AU NJIA ZA UVUTAJI
Zipo njia au mbinu kuu mbili ambazo hutumiwa na watumiaji ili kufikia mshindo wa ulevi.
1. Baada ya kumpata n'nge aliye komaa, wanamuweka Juani ili akauke, wengine hawatumii jua na wana kausha kwa makaa ya moto.
Baada ya n'nge kukauka wanasaga mabaki hayo na kisha kuvuta moshi kwa kutumia mrija kuelekeza puani.
2. Kunyonga au kuunda msokoto, Wengine wanaunda msokoto na kuchanganya mabaki ya nge ambayo yamesagwa na kuwa kama unga, kisha wana changanya na bangi kisha wanavuta.
Kutokana na vitendo hivi, wapo baadhi ya watu katika maeneo hayo wameona fursa na kuanza kuwatunza au kuwafuga wadudu hao na kisha kuwageuza kuwa biashara kwa kuwauzia waraibu wa ulevi huo.
Kutokana na kukosekana au ufinyu wa upatikanaji wa madawa ya kulevya ambayo yana gharama kubwa, wanatumia njia hii mbadala ambayo ni hatari zaidi kuliko madawa mengine, wengi wanakufa kwani sumu ni kali na huathiri mwili kwa kipindi kifupi.
Kadri siku zinavyozidi kwenda, dunia inashuhudia mbinu mpya za uraibu na matumizi ya madawa hatarishi zaidi.
Huku kwetu tumeona baadhi ya vijana wakitumia taulo za kike kwa matumizi ya pombe, huko kwa wenzetu nao wamekuja na style mpya ya ulevi, kuvuta sumu ya nge.