Kuwa kiongozi na ngozi nyeusi ni laana

Kuwa kiongozi na ngozi nyeusi ni laana

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,938
Reaction score
6,942
Juzi nilikuwa naelekea bunda kutokea Mwanza. Kuanzia Magu hadi bunda, mashamba ya mahindi yote yaliyo kando ya ziwa Victoria yamekauka kwa kukosa mvua, mengine yako chini ya mita 100 toka ziwani.

Nilianza kufikiria, hivi tunahitaji bilion ngapi ili mashamba yote yaliyo kando ya ziwa victoria pande zote za barabara yaanze kulima kilimo cha umwagiliaji?

Tuna laana sana na serikali haina mpango wa kufuta umaskini wetu. Hatuko serious na maisha hetu wenyewe.

Tuna maziwa makuu, mito mikubwa lkn vyanzo vya maji tena ya baridi kwa kilimo havijatumika halafu w wanatokea watu wanajifanya wanatupenda kweli?

Ujinga mtupu, hatuna dhamira ya kujikwamua.
IMG-20230224-WA0037.jpg
 
Juzi nilikuwa naelekea bunda kutokea Mwanza. Kuanzia Magu hadi bunda, mashamba ya mahindi yote yaliyo kando ya ziwa Victoria yamekauka kwa kukosa mvua, mengine yako chini ya mita 100 toka ziwani.

Nilianza kufikiria, hivi tunahitaji bilion ngapi ili mashamba yote yaliyo kando ya ziwa victoria pande zote za barabara yaanze kulima kilimo cha umwagiliaji?

Tuna laana sana na serikali haina mpango wa kufuta umaskini wetu. Hatuko serious na maisha hetu wenyewe.

Tuna maziwa makuu, mito mikubwa lkn vyanzo vya maji tena ya baridi kwa kilimo havijatumika halafu w wanatokea watu wanajifanya wanatupenda kweli?

Ujinga mtupu, hatuna dhamira ya kujikwamua.View attachment 2528348
Kukaa karibu na mahakama sio kujua sheria, kuna watu hapa pwani karibu na bahari kuu ila wanakosa mboga wana kula mihogo mikavu.....
 
Uvuvi ni suala lingine. Lkn tuna shida sana
 
Yaani watu waache kununua mabus wakae wawaze sijui umwagiliaji.
Waambie wakasombe maji ziwani kwa ndoo wamwagilie mahindi
 
Kukaa karibu na mahakama sio kujua sheria, kuna watu hapa pwani karibu na bahari kuu ila wanakosa mboga wana kula mihogo mikavu.....
Mahakamani hawafundishi sheria,pale sheria inatumika,
Na kama umebahatika kusoma sheria,mahakamani ni sehemu nzuri ya kujifunzia jinsi sheria inavyofanya kazi,hata kama ni raia Kuna kitu utqjifunza ukiwa unaenda mahakamani,kama sio mbali,Ili kujua taratibu za mienendo ya sheria.
Yes,haingii akilini jamii iishi Karibu na bahari,harafu ikose afya Bora ya mboga ya samaki,
Hapa ni mipango tu,kwa nini wasikopeshwe mitumbwi,wavue samaki,walipe ushuru kwa Kijiji maisha yaende.
 
Akianza kumwagilia tu, utasikia mambo ya uchafuzi wa mazingira, mara samaki wanakufa kwa kupata masalia ya mbolea n.k
 
Back
Top Bottom