Kuwa makini na vitu hivi wakati gari yako ipo kwenye matengenezo

Vocal Fremitus

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Posts
1,287
Reaction score
6,648
Ni kweli baadhi ya mafundi siyo waamifu..

Hivyo unatakiwa kuwa na utaratibu huu.. ili gari yako iwe salama pindi inapokuwa gareji..

1. Kuwa na sehemu maalumu ya kufanyia service Gari yako

2. Hakikisha gari yako inafanyiwa service katika mazingira yenye usalama na yanayoendana na thamani ya Gari yako..

3. Endapo matengenezo yanachukua muda mrefu ni vema kuandikishana vitu vyote vilivyomo ndani na nje ya Gari..

4. Wizi wa masega ndiyo kesi zinazoongoza kwenye magereji...hivyo Hakikisha unamkabidhi fundi wako... Na ukirudi ukague vibuyu vyote..

5. Baaadhi ya wamiliki huwa wanatelekeza kwa muda mrefu magari yao gereji... hii haipo sawa..

6. Service ndogo ndogo Kama za kubadilisha oil unatakiwa mwenyewe uwepo maana huwa hazichukui muda mrefu....lakini pia utakuwa na amani kwa sababu utakuwa unaona kila kitu...

7. Ogopa Sana zile gereji wanafanya kazi zao bila kukushirikisha...

Unapeleka gari gereji...halafu unaambiwa huruhusiwi kuingia huku[emoji38]

Mmiliki au Fundi garage unaezingatia haya tunaomba tukufaham.

C&P from unknown source
 
Sahihi kabisa
 
Gari inapigwa rangi huko painting Booth, will you be there? Hata kama sehemu inayopigwa rangi ni ndogo tu?
 

Wajinga wanatupiga sana oil filter 80K? Sema hizo bei zina VAT pale huwezi kwepa kodi.

12. Wheel balance
13. Wheel allignment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…