Kuwa makini sana na watu wa aina hii majuto yasiwe sehemu ya maisha yako

Kuwa makini sana na watu wa aina hii majuto yasiwe sehemu ya maisha yako

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
1. MUONGOPE SANA MTU ANAYEWEZA KUMKANA MTOTO WAKE KWA AJILI YA MAHUSIANO wapo watu hudiriki kuwakana watoto wao kwa ajili ya mahusiano au kuwaficha watoto hataki kusema kama ana watoto au anamkana lengo awe na mahusiano

2. MUONGOPE SANA MTU YULE AKIKOSA ALICHOKUOMBA ANASUSA AU ANATISHIA KUACHANA wapo watu wapo na wewe kwasababu fulanifulani tu si kwa upendo. Utajuaje atakuwa anasusa au kukutishia kuachana usimpompa alichotaka kwako. Jua HAMNAMO mtu hapo unatumika kama faraja au kutatua changamoto zake na atakuacha tu

3. MWANAUME ANAYEISHI NA MLINZI AU KIJANA WA KIUME KWENYE NYUMBA wapo wanaume kwasababu ya ndoa za masafa au hulka zake tu hupanga nyumba zima iliyojitenga au hujenga nyumba kisha huajiri mlinzi, shambaboy au huishi na jamaa wa kiume kwasababu yapo mambo hatayafanya akiwa na ndugu wa kike ndani. Mke na watoto wako Songea yeye anafanya kazi Bukoba anaishi na mlinzi au kijana wa kiume ambaye kazi yake ni kula na kufungua geti. Unaaminishwa hana ndoa au aliachana mke wake ndio maana amehamia hapo ukajiachia dada wa watu ukihisi umepata kumbe umepatikana utatumika kwa niaba ya mke wake na mwisho utaambiwa wazazi wamesema warudieane kumbe walikuwa mbalimbali wewe ukatumika kipozeo.

4. MTU ALIYEZAA WATOTO TABAKATABAKA kila mtoto na mama au baba ake bila hata sababu ya msingi. Waza mtu wa kwanza alikuwa mbaya, wapili mbaya na watatu mbaya yeye ni mwema sana. Kwa nini hakujisahihisha aliishi kwenye makosa yaleyale. Jitafakari kabla hujampa nafasi hiyo usije ukawa shamba darasa na wewe au ukatumika kulea watoto wake. Yawezekana mkwepa majukumu au mtu mwenye tamaa sana ndio maana anazaa hovyo

5. RAFIKI MUONGOPE SANA MTU ANAYETIA HURUMA wapo watu ukikutana naye yeye hulazimika tu hajawahi kupata mwenye upendo anajihesabia haki. Ukamuonea huruma ukaihisi anamanisha wapo watu ni wabaya sana kwenye uhalisia ila kwenye kuongea utahisi ni watu wanaojitaji kupendwa kumbe ni WAGALATIA watupu. Usimpende kwasababu anatia huruma anayejiona ni mwema sana.

6. MUONGOPE NA MKIMBIE MWANAUME ANAYEKUFUNDISHA ULEVI mara nyingi mwanaume huwa hapendi kuoa mwanamke mlevi ina anaweza kutumia kwa starehe zake ila siku akitaka kuoa anaoa asiye mlevi

7. MUOGOPE SANA MTU ANAYETAKA KINYUME NA MAUMBILE ukikutana na mtu anayetaka tendo kinyume na maumbile HAMNAMO mtu hapo. Usihisi ni sehemu ya upendo utaharibikiwa wewe MGALATIA na atakuharibu kisha ataenda kwa mwingine asiyefanya huo ujunga aliokufundisha

8. DADA ANGU MUOGOPE SANA MTU ANAYEKUAMBIA TUZAE KWANZA KABLA YA NDOA ukifanya hivyo umebet timu zote zifungane yaani unaweza ukawa single mother wa kujitakia na ukajilaumu maisha yako yote

9. DADA ANGU USIKUBALI MAISHA SOGEA TUISHI KAMA UNAIPENDA KESHO YAKO dada angu usijaribu utatumika na utazalishwa na kuachwa ukiwa umechakaa, huna nuru kabisa

Tukutane kwenye magroup yangu ya WhatsApp

Kaka Milton Tunge
0676151067
 
Hapo namba 6 sijakuelewa,umesema aogopwe mtu anayekufundisha ulevi au mtu anayekunywa pombe?na inawezekana vipi ukafundishwa kunywa pombe na mtu asiyekunywa,na unasema mwisho wa siku atakuacha aoe asiyekunywa,inawezekana vipi mwanaume anakunywa pombe halafu anataka kuoa mwanamke asiyekunywa...?
 
Mkuu ushauri umebase kwa wanawake sio?
 
Back
Top Bottom