Kuwa mpinzani sio ujanja na kuwa CCM sio ujinga , bila fair political battle ground chuki itatumaliza

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
CCM , CHADEMA,NCCR MAGEUZI na vyama vingine vyote vinaundwa na watanzania ingawa hawa watanzania wanakuwa na mitazamo tofauti kulingana na sera za vyama vyao .

Kipindi nakua nlikuwa naichukia sana CCM na kuwaona wale walio upinzani ndio wa maana sana ,nlikuja gundua yale ndio yalikuwa mawazo ya sisi wapinzani wengi .

Nlikuja gundua hata wanaCCM hawapendi ona mpinzani anapita , sasa hii sio siasa ni uadui na chuki .

Chuki ni mbaya sana lakini hii ilijengwa baada ya kuonekana CCM inaidiwa na dola au mfumo katika mambo mbali mbali .

Chuki inafanya hata CCM wakifanya vizuri ukosoa , Chuki inafanya kila anachofanya mbowe,zitto au lissu kionekane kizuri .

Chuki inafanya akitekwa wa CCM au wa CHADEMA ufurahie

Chuki ndio chanzo cha hizi kuuana ,kutesana , kutekana kutokana na tofauti za kisiasa.

Kwa hali ilivyo bila political fairness hali itakuwa mbaya zaidi , Serikali itengeneza fair political battle grounds .​
 
The chief cause of human errors is to be found in the prejudices picked up in childhood.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…