Nsennah
JF-Expert Member
- Jan 9, 2021
- 1,947
- 1,554
Mwanzo
Tanzania ni nchi ya muungano wa kipekee duniani ambayo serikali yake inaundwa na mihimili mitatu yaani Serikali kuu, Bunge na Mahakama. Bunge kama chombo mhimu cha kutunga sheria na kuisimamia serikali ili kuleta tija na msitakabali mkubwa wa maendeleo ya nchi linapaswa kuwa ni sauti ya umma. Ili kuimarisha wajibu huu wa bunge, ni vyema bunge kama mhimili wa serikali ungepata wabunge wake kwa njia ya kipekee tofauti na mabunge mengine kama ilivyozoeleka duniani.
HALI YA SASA YA UPATIKANAJI WA WABUNGE
Chombo hiki kinajengwa na wawakilishi wa wananchi (wabunge) wanaopitishwa na vyama vya siasa kama wagombea na kupigiwa kura na wananchi wa majimbo husika pamoja na viti maalumu (katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 61 (1) na 77 (1),(2),(3)). Upatikanaji huu umekuwa ukididimiza utekelezaji wa majukumu yao kutokana na changamoto kadha wa kadha. Ili kuelekea Tanzania tuitakayo kwa miaka 5 hadi 25 ijayo ni mhimu kukabiliana na changamoto hizo.
Changamoto
*Kutokuwepo kwa usawa katika kuhudumia majimbo ya uchaguzi. Ni dhahiri kuwa mmoja wa viongozi yeye alitamka wazi wazi (pengine wengine walifanya hivyo kimya kimya) kuwa hawezi kupeleka maendeleo kwa jimbo ambalo mbunge wake hatokani na chama chake.
www.jamiiforums.com
*Wabunge kusimamia msimamo wa chama kuliko msimamo wa wananchi. Kumekuwa na matukio mengi yakionesha wazi wabunge kushindwa kusimama na uhalisia wa kimaamzi kwa kuwa si msimamo wa chama.
View: https://youtu.be/1t18IurlnLY?si=gP9x8QUqoXxbdGf1
*Bunge kushindwa kutekeleza kikamilifu shughuli zake. Uwepo wa kauli kutoka kwa ofsi za serikali zinazoonesha madhaifu ya bunge letu katika utekelezaji wa shughuli zake kwa sababu mbalimbali ikiwemo mwamvuli wa vyama.
*Rushwa hasa wakati wa kura za maoni. kumekuwepo na matukio ya rushwa katika upitishaji wa wagombea ndani ya vyama kwenda kwa wajumbe wahusika hivyo wananchi kupelekewa wagombea wasio waadilifu
MAPENDEKEZO KUELEKEA TANZANIA TUITAKAYO
Ili kupunguza ama kuondoa kabisa changamoto zilizoanishwa hapo juu na hatimaye kuipata Tanzania tuitakayo kwa miaka 5 hadi 25 ijayo ni vyema tukafanya yafuatayo.
1. Kurekebisha kifungu cha katiba kuhusu upatikanaji wa wabunge. Ni vyema wabunge wangepatikana kama wagombea binafsi wanaofanyiwa usaili na kupitishwa na baraza la madiwani wa jimbo husika kwa idadi isiyozidi pendekezo la katiba na baadaye wananchi wachague yupi anastahili kuwa mwakilishi wao bungeni.
2. Kudumisha uhuru wa bunge katika kutekeleza majukumu yake. Katiba lazima iimarishe kwa umadhubuti majukumu ya bunge na uhuru wake katika utekelezaji wa majukumu yake bila kuathiriwa na mhimili mwingine wowote wa serikali.
3. Kupitia upya majukumu ya bunge. Ni wazi kuwa shughuli ama majukumu ya bunge yapo kikatiba hivyo ni mhimu kuyatazama upya aidha kwa kuyapunguza, kuongeza au kurekebisha majukumu yake kama mhimili wa nchi.
4. Kuwalinda na kuwaheshimu wabunge wanaotekeleza majukumu yao ya kibunge. Upo ushahidi wa vitisho na majaribio kadha wa kadha ya kupigwa risasi baadhi ya wabunge mf. Tundu Lissu na Christopher Ole Sendeka, mambo ambayo yanayowarudisha nyuma wabunge katika kutekeleza majukumu yao.
5. Vyama vya siasa vipewe nafasi ya wawakilishi bungeni. Ili kudumisha mfumo wa vyama vingi, ni vizuri vyama vitano bora vitakavyoongoza kwa idadi kubwa ya madiwani vikapewa nafasi ya kutoa wawakilishi walau 10 kila chama kuwa wabunge kupitia vyama vyao kwa mchakato wa ndani wa chama kwa njia ya kidemokrasia.
Hitimisho
Tanzania tuitakayo ni lazima iwe yenye mhimili wa bunge ulio madhubuti kwani ndio unasimamia serikali katika utekelezaji wa miradi, kujadili mikataba kwa maslahi ya nchi, unaohoji madhaifu ya watendaji na kuibua ubadilifu wa fedha pamoja na rasilimali za nchi unaofanywa na watendaji wa serikali kuu. Bunge imara ni chachu ya kuwa na uongozi wenye uwajibikaji, uwazi na wenye kuheshimu haki za raia kwa kutoa huduma bora kwa wananchi. Hata hivyo, uchaguzi kupitia vyama vya siasa ubaki wa serikali za mtaa, madiwani na rais atakayeunda baraza lake la mawaziri. Bunge litokane na wagombea huru na mahakama ibaki ya wanasheria ili kutoa haki. Mwisho japo si kwa mhimu, Tanzania ni yetu sote inayohitaji mshikamano kama taifa bila kujali dini, chama, rangi, kabila wa ukanda hivyo maamzi yatendeke bila kufungamana na upande wowote. Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi 2020 - Sera ya kutopeleka maendeleo Majimbo ya Upinzani inahalalisha Sera ya Majimbo!
Sera mojawapo ya CHADEMA ni majimbo. Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri. Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee...
*Wabunge kusimamia msimamo wa chama kuliko msimamo wa wananchi. Kumekuwa na matukio mengi yakionesha wazi wabunge kushindwa kusimama na uhalisia wa kimaamzi kwa kuwa si msimamo wa chama.
View: https://youtu.be/1t18IurlnLY?si=gP9x8QUqoXxbdGf1
*Bunge kushindwa kutekeleza kikamilifu shughuli zake. Uwepo wa kauli kutoka kwa ofsi za serikali zinazoonesha madhaifu ya bunge letu katika utekelezaji wa shughuli zake kwa sababu mbalimbali ikiwemo mwamvuli wa vyama.
*Rushwa hasa wakati wa kura za maoni. kumekuwepo na matukio ya rushwa katika upitishaji wa wagombea ndani ya vyama kwenda kwa wajumbe wahusika hivyo wananchi kupelekewa wagombea wasio waadilifu
*Utumiaji mbaya wa vyombo vya dola kulinda maslahi ya chama chenye nguvu kisiasa Kutokana na wagombea kutokana na vyama vya siasa, kumekuwepo na malalamiko ya baadhi ya wagombea kutoka vyama tofauti kufanyiwa ukatili na vyombo vya ulinzi na usalama.
*Uporaji wa kura ili chama fulani kupata ushindi. Ni wazi matukio haya yamekuwa kero kwa wagombea wa vyama tofauti tofauti hivyo kupatikana kwa mbunge asiyekuwa chaguo halali la wananchi
*Bunge kuingiliwa na mhimili mwingine. Kumekuwepo na viashiria vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuingiliwa na serikali kuu hivyo kupunguza ufanisi wa chombo hiki (rejea swali la Pascal Mayalla kwa rais wa awamu ya 5). Pia waziri ambaye ni mbunge kutokuwa na uwezo wa kuhoji bungeni changamoto zilizopo kisa yuko kwenye baraza la mawaziri ambao ni watekelezaji wa shughuli za serikali kuu.*Uporaji wa kura ili chama fulani kupata ushindi. Ni wazi matukio haya yamekuwa kero kwa wagombea wa vyama tofauti tofauti hivyo kupatikana kwa mbunge asiyekuwa chaguo halali la wananchi

Upvote
0