Wadau mi naona kuwa na rafiki wa kike ambaye si
mpenzi wangu inaniwia ngumu sana sasa sijui ni
mimi tu au hata nyie inakua hivyo hivyo .
maana unaweza kukuta unae rafiki wa disign hiyo halafu ukamtumia
sms jamaa yake akajua unatangaza nia kumbe ni rafiki tu.....
Hebu peleka mapenzi yako kule kunakostahili. Hapa tunajadili mambo ya Kitaifa siyo ngono!!
hakuna urafiki kati ya mtoto wa kiume na wa kike unless mmoja wao awe gay au lesbian; period!
binafsi mawazo yangu ndio hayo hakuna urafiki kati ya mwanamke na mwanaume lazima kutakuwa na matamanio tu
Tatizo sio kwa sisi tunaokuwa na marafiki wa kike bila kuchanganya mapenzi na urafiki, bali kwa wanaotuzunguka ambao tayari wana imani kuwa ama utakuwa unamtafuna, angalau unadowea au uko bwabwa.
Nilipokuwa katika nchi ambazo huwa hawafkirii hivyo, nilikuwa na marafiki wa kike na kule tuliishi bila shutuma, lakini siku mmoja wao alipokuja kunitembelea, maneno maneno yakaanza. Kusema kweli niliabika kwani wengine walithubutu hata kumweleza bayana kuwa ni mchuchu wangu. Mwaka uliofuatia walikuja wanne kwa mpigo watu nyumbani washindwa kusema kama wote ninawatafuna.
Ninachotaka kusema ni kuwa ninakubaliana na hali kuwa katika jamii zetu urafiki baina ya wanaume na wanawake hauangaliwi kwa jicho zuri, kwa ile imani kuwa "mwanamume mkabidhi mamilioni akuwekee amana atazihifadhi lakini ukimwacha na mwanmke japo kwa dakika moja atajaribu angalau kulenga mshipi"
Hilo si swala la watu kufikiri hivyo tu; ni swala la ki biolojia. Wewe utakuwa ni exceptional. Na huwezi kuusemea moyo wa mtu mwingine; wewe waweza sema they were just friends ( or we are just friends) kumbe hao mabinti walikuwa wanakusubili kwa hamu uwakisi tu mmalizane.
Haya mambo hayana cha ulaya wala afrika, hakuna urafiki kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Sema huku afrika watu watasema sana ulaya na nchi za west hakuna anayejali huko na nani (at least kinafiki) ; but ukweli unabaki pale pale.
Na wakati mwingine unakuja kugundua kuwa unamfeel mtu pale utakapomwona yuko na lover wake; karoho kanaanza kudunda wakti you were just friends.
Kuna kijana alikuwa mshkaji wangu wa kawaida college; lakini alitaka kuzichapa na jamaa aliyekuwa ananifukuzia; wakati hatukuwa lovers. Namuuliza nini; anasema jamaa player huyu hakufai. Inahuu
urafiki wa paka na samaki huwa ni wa mashaka sana....
yap ! Punguzen matamanio waweza kuwa nao bila mapenzi.
Bila shaka wazungu wana wivu, mara nyingi wanapigana kwenye kumbi za starehe na mitaani kwa wivu, tafauti ni jinsi ya kuheshimu urafiki mpaka uliopo baina yao. Kwa nini usimchukulie rafiki yako wa jinsia tafauti kama ndugu yako, harimu yako? Ninakubali kuwa, iwe mwanamke au mwanamume, mmoja anapokuwa mbele ya wa jinsia tafauti "anaweza" kuwa na hizo feelings za kibiolojia, anaweza kuona wivu, na kama ana hisia za mapenzi, mapenzi yake yataishia kuwa ni "Platonic, Impossible, Prohibited Love", kwa ajili ya heshima na kujali urafiki. Katu huwezi kuuamua kuupoteza urafiki huo kwa ashki za kupita.Hilo si swala la watu kufikiri hivyo tu; ni swala la ki biolojia. Wewe utakuwa ni exceptional. Na huwezi kuusemea moyo wa mtu mwingine; wewe waweza sema they were just friends ( or we are just friends) kumbe hao mabinti walikuwa wanakusubili kwa hamu uwakisi tu mmalizane.
Haya mambo hayana cha ulaya wala afrika, hakuna urafiki kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Sema huku afrika watu watasema sana ulaya na nchi za west hakuna anayejali huko na nani (at least kinafiki) ; but ukweli unabaki pale pale.
Na wakati mwingine unakuja kugundua kuwa unamfeel mtu pale utakapomwona yuko na lover wake; karoho kanaanza kudunda wakti you were just friends.
Kuna kijana alikuwa mshkaji wangu wa kawaida college; lakini alitaka kuzichapa na jamaa aliyekuwa ananifukuzia; wakati hatukuwa lovers. Namuuliza nini; anasema jamaa player huyu hakufai. Inahuu