Najaribu kufikiria umuhimu wa kuwa na demokrasia sijaweza kupata jibu. Kwa kuwa nchi hii inakuwa na chaguzi kila baadaya ya miaka mitano
na kwa kuwa baadhi ya viongozi wengi wamekuwa wakipata madaraka mara nyingi
zaidi ya hata miaka kumi kwa wabunge na miaka 10 kwa nafasi ya urais. Na kwa kuwa hali hiyo inajidhihirisha tena mwaka huu
Je si wakati muafaka sasa kuona kwamba tuwe na viongozi wa maisha tuizike demokrasia ambayo kimsingi haipo Tanzania? Na kwa kuwa kuna gharama kubwa za chaguzi hizi, Je si busara kuacha hao walioteuliwa kuendelea kutuongoza ili hizo gharama zitumike kwa mambo mengine ya maendeleo? Kuna haja gani basi ya kuwa na chaguzi wakati wale wale tusiowataka ndio wanakuwa viongozi wetu
Tujadili kwa busara
Siku Ya Wajinga kwisheni.